FUATILIA HAPA TUKIO ZIMA LA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA LEO,MABILIONI YA FEDHA YAPITISHWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015 KWA AJILI YA MANISPAA HIYO

Aliyesimama ni mwenyekiti wa baraza la madiwani katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila akifungua kikao kwa ajili ya kupitisha bajeti ya halmashauri hiyo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo mjini Shinyanga.Wa kwanza kulia ni katibu tawala wa mkoa  ndugu Anselim Tarimo,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu  Anna Rose Nyamubi ,akifuatiwa na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga ndugu Festo Kang'ombe wakifuatilia alichokuwa anazungumza mwenyekiti wa kikao hicho wakati wa kufungua kikao


Awali mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang'ombe akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mapato na matumizi katika manispaa hiyo katika mwaka wa fedha 2014/2015 ambapo manispaa hiyo inatarajia kupata jumla ya shilingi 24,550,984,864=.Katika fedha hizo makusanyo ya ndani ya manispaa ni shilingi 2,224,153,200/=,ruzuku kutoka serikalini 14,564,193,840/=.Alisema bajeti hiyo pamoja na mambo mengine inalenga katika kutekeleza malengo ya mpango wa matokeo makubwa sasa- BIG RESULT NOW
Wajumbe katika baraza hilio wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika kikao hicho ambapo baada kuwasilishwa kwa rasimu ya bajeti hiyo walijadili mapungufu ya bajeti na baadaye kuipitisha.Aidha baadhi ya wajumbe hao waliomba bajeti hiyo pia iguse makundi maalum kama vile watoto ,walemavu na wazee,lakini pia wengine waliomba pia suala la wenyeviti wa mitaa,vitongoji na vijiji waangaliwe kwa jicho la huruma kwani hivi sasa wanalipwa posho ya shilingi elfu 10 kwa mwezi wakati wanafanya kazi kubwa hivyo kuonekana kuwa hawatendewi haki.


Wajumbe wa kikao hicho walihoji kuhusu matangazo,mabango na ushuru wa aina  mbalimbali jinsi unavyonuifaisha  manispaa ya Shinyanga,lakini pia wakagusia kuhusu michango ya mara kwa mara katika shule mfano katika baadhi ya shule za sekondari kila mwaka mwanafunzi anadaiwa pesa ya dawati,mafyekeo hali a,mbayo walisema inatokana na baadhi ya wakuu wa shule kutokuwa waaminifu

Mwenyekiti wa kikao hicho David Nkulila akizumgumza katika kikao hicho ambapo alisema katika kutekeleza bajeti hiyo suala la siasa linapaswa kuachwa na kuwa wakweli na kuwataka kuwa wakali katika kusimamia ukusanyaji wa mapato pamoja na kwamba kuna changamoto kubwa katika kufikia mafanikio akawaomba  pia wananchi kuwasikiliza viongozi wao ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo

Kikao kinaendelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post