Katibu wa
siasa na uenezi wa CHADEMA taifa John Mnyika akizungumza mjini Shinyanga baada ya kutoka Kahama ambapo Chopa yao waliyokuwa wanaitumia kupotea katika eneo la Ubagwe
hivyo hawakufanikiwa kufika katika eneo hilo walikopaswa
kufanya mkutano ambapo uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani unatarajiwa
kufanyika kutokana helikopta waliyokuwa wakitumia kupotea njia na kutua sehemu
nyingine na hivyo kufanya safari yao kuihairisha na kuelekea mjini Shinyanga
kwa ajili ya mkutano na wananchi.
Chama cha Demokrasia
na Maendeleo nchini kimemkataa diwani wake wa Kata ya Majengo wilayani Kahama mkoani
Shinyanga Bobson Wambura kwa madai kuwa ni msaliti na anahujumu chama hicho.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara mjini Kahama mkoani Shinyanga katibu wa siasa na uenezi
wa Chadema taifa John Mnyika katika moja ya mikutano ya chama hicho ijulikanayo
kama Operesheni
Pamoja Daima alisema hawatakubali
katika chama chao kuwa na watendaji wasaliti.
Alisema hivi
sasa wapo katika kazi ya kuwaondoa watu kama Diwani huyo wa kata ya Majengo ambaye
walimwita ni msaliti mkubwa wa chama hicho na alipaswa kuondolewa kabisa kwenye
chama hicho.
Mnyika
alisema moja ya sababu zilizofanya diwani huyo kuondolewa katika chama hicho ni
madai ya kwamba alishiriki katika kufanikisha chama hicho kisipeleke mgombea
udiwani katika kata ya Ubagwe wilayani Kahama katika uchaguzi wa mdogo wa
udiwani unaotarajiwa kufanyika kutokana na aliyekuwa diwani wa kata hiyo Robert
Mndula kufariki dunia mwaka jana.
Aliitaja
sababu nyingine kuwa ni madai ya kuwa diwani huyo alikuwa akizunguka mitaani na
kuwaambia watu kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA walitoa kiasi cha shilingi
milioni tano ili kuwashinikiza wananchi wahudhurie katika mkutano JANA wa chama
hicho mjini Kahama.
“Mimi ndiye
katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo hapa nchini na Bobson ni
Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Kahama je, Wananchi mnaniruhusu nimwondoe diwani
huyo”, alihoji Mnyika.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwa njia ya simu akiwa jijini Mwanza Diwani wa Kata ya
Majengo Bobson Wambura alisema tuhuma hizo siyo za kweli na kwamba viongozi wa
Chadema wameamua kufanya hivyo kwa ajili msimamo wake na aliyekuwa naibu katibu
mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.
“Zitto Kabwe
ni rafiki yangu iwe ndani ya chama au nje ya chama na nipo tayari kwa lolote
watakaloamua wenyewe mimi Chadema siyo yangu kwani hapo zamani nilikuwa naishi
kwa udiwani au chama?”, alisema Wambura.
Post a Comment