Mhh!! BIBI ANAYESADIKIWA KUWA MCHAWI AKUTWA CHUMBANI KWA MTU,AKIWA UCHI Bi. Kizee akiwa kwenye gari la polisi baada ya kuokolewa na polisi kutoka kwa wananchi wenye asila kali mara tu ya kukutwa kwenye chumba.
 Bi. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi  amenusurika kifo baada ya polisi kumnusuru kwa kudaiwa kukutwa akiwa uchi chumbani kwa mtu  akifanya mambo yasiyoeleweka alfajiri ya leo  Ijumaa Januari 31,2014
Mashuhuda wa mwanzo wanasema Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua la kufanya huku mwili wake ukiwa Uchi na nguo zake  zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni  mchawi wakati wengine wakisema wasubiri taarifa ya Polisi.
 Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na  Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa watu waliomkurupusha bibi huyo chumbani.
 Wakielekea kituo cha cha polisi cha Bukoba Mjini leo asubuhi.
 Bibi huyo akiwa kwenye ulinzi mkali baada ya kufikishwa kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Bukoba

PICHA ZOTE NA BUKOBAWADAU BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post