Utapeli !!! BAADHI YA MAWAKALA WA AIRTEL MONEY WAANZA KUTAPELI WATEJA HUKO NZEGA

Baadhi ya mawakala wa AIRTEL MONEY katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora wamegeuka kuwa matapeli hususani katika maeneo ya vijijini ambapo pamoja na kampuni ya airtel kutangaza kuwa 'TUMA NA KUTOA PESA BURE BILA KIKOMO" ,kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao wa  malunde blog umezinyaka ni kwamba katika maeneo ya vijijini ambako wakati mwingine kuna wakala mmoja pekee,hali imekuwa kinyume kwani mawakala hao wamekuwa wakifanya mambo kinyume ambapo pindi mteja anapohitaji kutoa shilingi elfu kumi,hupewa shilingi elfu tisa badala ya elfu kumi,na unapotaka kutoa shilingi elfu 50 wateja hao hulazimika kukatwa shilingi 2000 hadi 2500.

Akizungumza na malunde blog mmoja kati ya wateja hao ambaye hakutaka jina lake lijulikane amesema kutokana na kwamba katika kijiji chake kuna wakala mmoja (Jina tunalo) wamekuwa wakilazimika kukatwa pesa zao pamoja na KWAMBA HAKATWI MTU HAPA kutokana na ujanjaujanja wa wakala huyo,lakini sasa hivi wameanza kumwogopa wakala huyo na kulazimika kusafiri kutoka kijijini hapo  umbali wa takribani saa moja kwa baiskeli kwenda eneo la Nata kufuata huduma hiyo .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post