Shinyanga noumaa!!!! WENYE MPANGO WA KUFANYA UHALIFU MSIMU HUU WA SIKUKUU KUANGUKIA MIKONONI MWA POLISI

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala

 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limesema katika kuhakikisha wanachi wake wanasherehekea sikukuu ya chrismas na mwaka mpya limeandaa vikosi kazi kwa ajili ya kukabiliana na wahalifu wanaotumia msimu wa sikukuu kufanya uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo kuvamia na kupora mali za wananchi

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema vikosi kazi hivyo vitasambaa kila wilaya vikifanya doria na msako mkali ili kuhakikisha kuwa wananchi wanasherehekea sikukuu kwa amani na utulivu

“Mwaka huu tumeamua kuja na staili yetu hapa Shinyanga kwani katika msimu wa sikukuu wahalifu  wamekuwa wakipanga mbinu za kuvamia majumbani kwa wananchi  kwa lengo la kuwapora mali ,na
 na vikosi kazi hivi vitafanya kazi hadi mwezi wa kwanza”,aliongeza Kamanda.

 Kamanda Mangala ametumia fursa hiyo kuwaonya  watu wanaomiliki silaha kihali na kutumia kinyume na taratibu mfano kujeruhi na kutishia wenzao jeshi  la polisi halitasita kunyang’anya silaha kwa kufuata taratibu na sheria.

Aidha  amewataka wananchi  pindi wanapokwenda kwenye sehemu za starehe wasiache nyumba zao pekee bila ya kuwa na mwangalizi ili kutowapa mianya wahalifu kupora mali zao na kutoa taarifa pindi wanapohisi kuna uvunjifu wa amani unataka kufanyika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post