Nguo za kutamanishana marufuku !! WABUNGE WAPIGA MARUFUKU UVAAJI WA MINISKIRTS NCHINI UGANDA,MASHOGA KIFUNGO CHA MAISHA AU KIFOWabunge wa nchini Uganda leo wameupitisha muswada wa ‘anti-pornography’ utakaopiga 

marufuku uvaaji miniskirts na nguo zingine zinazotamanisha kimapenzi. Muswada huo unaopingwa vikali kama tishio kwa haki za wanawake unaweza kufanya filamu nyingi na tamthilia kupigwa marufuku.

Wengine wanasema muswada huo unaweza kuzuia video nyingi za wasanii kama Beyonce ama Rihanna kuchezwa kwenye runinga za nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor muswada huo unapiga marufuku kitu chochote kinachoonesha sehemu za faragha kama matiti, mapaja na makalio ama tabia yoyote inayoweza kuamsha hisia za mapenzi au tabia yoyote inayoenda kinyume na maadili.

Muswada huo umekuja kufuatia kuongezeka kwa masuala ya pornography nchini Uganda ni marudio ya kile kilichofanyika wakati wa uongozi wa Idi Amin aliyepiga marufuku uvaaji wa sketi fupi miaka 1970s.

Leo pia wabunge wa nchi hiyo wamepitisha muswada wa kuzuia ushoga nchini humo.

 Muswada huo unapendekeza kifungo cha maisha kwa mashoga au kifo kwa wale wanaorudia makosa hayo. Kama muswada huo ukipita, mtu yeyote atakayeshindwa kumripoti mtu anayejulikana kuwa shoga naye anaweza kushtakiwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post