 |
Awali afisa biashara wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu(aliyesimama) bwana Mwafongo Konisaga akimkaribisha afisa habari,mawasiliano na uhusiano wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga John Mlyambate katika ukumbi wa mikutano wa wilaya hiyo wakati wa mkutano
wake na waandishi wa habari kuzungumzia hali halisi ya maendeleo katika wilaya
hiyo ambapo kituo kipya cha mabasi kitajengwa katika eneo la kijiji cha Isoso kata ya
Kishapu wilayani humo. |
 |
Afisa habari,mawasiliano na uhusiano wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga John Mlyambate akizungumza na waandishi wa habari leo ambapo amesema halmashauri ya wilaya ya Kishapu imeanza rasmi
ujenzi wa kituo hicho kwa kiwango cha changarawe mwezi Oktoba mwaka huu na utakamilika mwezi
Juni mwaka 2014 na hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni moja |
 |
Ni katika eneo la kijiji cha Isoso kata ya Kishapu kunakojengwa stendi ya mabasi yatokayo na kuingia katika wilaya ya Kishapu.Uchimbaji wa misingi kama unavyoona unaendelea |
 |
Misingi inaendelea kuchimbwa.Katika kituo hicho cha mabasi kutakuwa na zaidi ya vibanda 300 kwa ajili ya wafanyabiashara hivyo stendi hiyo itawanufaisha wakazi wa eneo hilo siyo tu kutatua kero ya usafiri lakini pia ajira |
wakazi wa wilaya hiyo kwa muda mrefu wamekosa eneo rasmi kwa ajili ya huduma ya usafiri hivyo
wakati mwingine wakijikuta wakikosa usafiri kutokana na kukosa eneo maalum kwa
ajili ya kusubiri usafiri.Ujenzi wa kituo hicho utakuwa neema kwao
Kwa mujibu wa afisa habari John Mlyambate mradi huo unajengwa kwa kutumia fedha ambazo
halmashauri imekopa kutoka bodi ya mikopo ya serikali za mitaa kiasi cha
shilingi 800,000,000/= ambapo halmashauri tayari imechangia shilingi
200,000,000/= ili kukamilisha thamani ya mradi huo ambapo ni shilingi bilioni
moja
 |
Tayari wakazi wa eneo hilo wameanza kunufaika na ujenzi huo.Hapo juu ni bi Kadogo Tophil ,mwanamke pekee ambapo kamera za Malunde Blog zilifanikiwa kumnasa akichimba msingi,ambapo kwa mujibu wa maelezo yake ukichimba umbali wa mita moja ,ikiwa urefu kwenda chini ni mita 2 na nusu unapatiwa shilingi elfu moja na yeye kwa siku ana uwezo wa kuchimba mita saba |
 |
Changarawe tayari zishaanza kusogezwa eneo la mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi katika wilaya hiyo |
 |
Hapa ni katika moja ya eneo la mji wa Mhunze wilayani Kishapu kama unavyoona hapo juu magari madogo yamepaki kutokana na kukosa eneo maalum kwa ajili ya kupaki.Hapo ni karibu na barabara ambako wakazi wa eneo hilo hulazimika kuvizia magari kwa ajili ya usafiri |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment