Mkurugenzi wa idara ya uratibu wa maafa kutoka ofisi ya
waziri mkuu,luteni jenerali Sylivester
Rioba mapema leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuijengea jamii uwezo wa kupunguza
athari za maafa kwa mikoa iliyoathirika
zaidi na ukame kama vile mkoa wa Kilimanjaro na Shinyanga,uzinduzi ambao
umefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu na Kishapu ndiyo wilaya pekee katika mkoa wa Shinyanga ambayo itanufaika na mradi huo unaofadhiliwa na benki ya dunia
|
Katibu tawala wa wilaya ya Kishapu bwana Octavian Mangosongo akizindua mradi huo kwa niaba ya mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambapo pamoja na mambo mengine utahusisha kuelimisha vijana na akina mama juu ya upndaji miti na
kilimo cha mazao yanayohili ukame hususani mihogo na viazi vitamu pamoja na kuaninisha na kutoa
mafunzo kwa wadau kuhusu matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo,mifugo na
misitu lakini pia upatikanaji wa maji safi na salama.
|
|
Aliyesimama ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu
bwana Justin Sheka akizungumza wakati wa uzinduzi ho wa mradi wa kuwawezesha wananchi katika kupunguza athari za maafa na katika wilaya ya Kishapu miradi ya ,majaribio itaanzia itafanyika katika kata ya Masanga na Mwamalasa .Sheka amesema kama mradi huo utatekelezwa ipasavyo utakuwa mkombozi wa maisha ya wakazi wa Shinyanga |
|
Wadau mbalimbali waliokuwepo wakati wa uzinduzi huo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu |
|
Wadau muda mchache baada ya uzinduzi wa mradi huo ambao unategemewa kuwa suluhisho la maafa mbalimbali katika wilaya hiyo kama vile ukame unaopelekea kuwepo kwa upungufu wa chakula wa mara kwa mara |
|
Baada ya uzinduzi huo,Picha ya pamoja kwa wadau waliohudhuria uzinduzi wakiwemo wakina mama,vijana,walimu wakuu,idara na asasi mbalimbali,wilaya na mkoa kwa ujumla,waandishi wa habari na wengine wengi |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553