MGEJA AWAFUNDA MAWAZIRI WANAOKWEPA OFISI ZA CCM HAPA NCHINI

NB PICHA KUTOKA MAKTABA YA MALUNDE
Mjumbe  wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  (NEC) Khamis Mgeja ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa  Shinyanga amewashauri baadhi ya mawaziri hapa nchini kuacha tabia ya kuzinyanyapaa ofisi za chama cha mapinduzi CCM pindi wanapokuwa katika ziara za kikazi katika wilaya na mikoa  kwani katika ofisi hizo ndipo  kwenye taarifa mbalimbali za kero za wananchi.

Akiwahutubia wanachama na wananchi  wakati wa ziara yake mkoani shinyanga mwishoni mwa wiki iliyopita amabpo Mgeja alisema baadhi ya mawaziri wanaofanya ziara za kikazi mikoani na wilayani wamekuwa na  tabia ya kukimbilia katika ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya na hata pale wanapokwenda katika ofisi za CCM huchungulia mara moja na kuondoka baada ya kuweka saini katika vitabu vya wageni badala ya kufika katika ofisi za chama na kusikiliza kero za wananchi.

Mgeja alisema endapo mawaziri watajenga utamaduni wa kufika katika ofisi za chama wataelezwa kero hizo, watapewa ushauri jinsi gani wazipatie utatuzi,na ushauri wa nini kifanyike katika kuboresha zaidi utendaji ndani ya wizara zao, lakini pia wataelezwa ni watendaji gani wa serikali katika wilaya ama mkoa wasiotimiza wajibu wao.

Mjumbe huyo wa NEC alisema ni vizuri mawaziri hao hivi sasa wakabadilika na waache kufanya kazi zao kwa mazoea hali ambayo itasababisha chama kihukumiwe kwa makosa ambayo siyo ya kwake, na lazima waelewe CCM hivi sasa imechoka kubeba mizigo ya lawama zinazotokana na uzembe wa baadhi ya mawaziri ndani ya serikali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post