Inatia kichefu chefu !!! TAZAMA HALI HALISI YA MAZINGIRA YA SOKO LA NGOKOLO MAARUFU NGOKOLO MITUMBANI MJINI SHINYANGA

Ni katikati ya soko la mitumba (gulio)maarufu kwa jina la soko la Ngokolo mitumbani mjini shinyanga,ambapo kila siku za JUMAMOSI huwa ni neema kwa wakazi wa eneo hilo.Kama unavyoona   ndiyo hali halisi katika soko hilo maji yametuama mithili ya bwawa na shughuli za kuuza na kununua bidhaa mbalimbali zikiendelea hapo jana Jumamosi,siku ambayo wakazi wengi wa shinyanga hufika eneo hilo kununua na kuuza kile wanachoona kinafaa

Hapa ni katika eneo jinmgine ndani ya soko la Ngokolo mitumbani ambapo malunde blog ilifanikiwa kupita katika soko hilo hilo pendwa kwa wakazi wa shinyanga

Hili pia ni eneo jingine ambapo maji yanayotokna na mvua yametuama.Wakizumza na mwandishi wa malunde blog wakazi wa eneo hilo walihoji kama hali hivi sasa iko hivi  wakati hakuna mvua kubwa je ikinyesha mvua kubwa hali itakuwaje?

Ndani ya soko hilo uchafu ni jambo la kawaida kabisa

 Dada hapo mbele mmoja wa wakazi wa shinyanga aliyekuwa katika soko hilo akijaribu kukwepa maji /matope ndani ya soko hilo
Hali ni tete,ukiteleza kidogo tu lazima uogelee
Biashara inaendelea

Nje ya soko hilo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

  1. Serikali ya maeneo hayo imechukua hatua gani jamani kuwaelimisha wananchi husika? Halafu kipindi hiki cha mvua pande hiyo na ndo kipindi cha kipindupindu, malaria, kuhara, n.k.

    ReplyDelete

Post a Comment