Breaking News!!!!! WATU WATANO WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUIBA RAMBIRAMBI GEITA,MMOJA KATI YAO AKATWA MGUU NA KUDUMBUKIZWA KISIMANI AKAFIA HUMO HUMO



NB -PICHA SIYO YA ENEO LA TUKIO

Na Valence Robert- Geita



Watu watano wamekufa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kutokana na kile kinachoelezwa kuiba rambirambi ya shilingi elfu 65 katika familia ya mzee Luhemeleja aliyekuwa amefiwa na mjukuu wake.

Tukio hilo limetokea leo mchana majira ya saa saba na nusu  katika kitongoji cha Nyantolotolo (A) nje kidogo ya mji wa Geita.

mashuhuda wa tukio hilo wamesema Mzee Luhemeja alifiwa na mjukuu wake na baada ya msiba huo kuisha hapo jana watu wote wakiwepo pia watuhumiwa wa tukio hilo walisambaa na kurudi makwao.

Mashuhuda wameongeza kuwa jana usiku  watu wapatao wanane walifika nyunbani kwa mzee huyo kulikotokea msiba huo na kuingia ndani ambapo walimkuta mtoto mdogo na kumpiga kofi baadae wakamfuata mzee wakampiga na kumuonba awapatie fedha kwa usalama wake.

Baada ya kumpiga mzee huyo watuhumiwa walifanikiwa kuchukua shilingi elfu 60 zinazodaiwa kuwa ni  pesa za rambirambi zilizotolewa wakati wa msiba baada ya mzee huyo kufiwa na mjukuu wake.

Imeelezwa kuwa baada ya kuchukua pesa kwa mzee watuhumiwa hao na walimfuata mke wa mzee huyo ambaye jina lake halijafahamika naye wakampiga na kumuumiza kisha  kuchukua kiasi cha shilingi elfu 5 toka kwake kisha wakatokomea kusikojulikana 

Baada taarifa kusambaa kuwa kuna uvamizi umetokea ,jeshi la jadi sungusungu lilianza msako na kufanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa akiwa na damu kwenye nguo zake na  kumhoji juu ya tukio hilo, mtuhumiwa akaanza kuwataja wenzake mmoja baada ya mwingine na jeshi hilo kuwatia mbaroni wote watano.

Baada ya watuhumiwa kutiwa  mbaroni wananchi wenye hasira kali walianza kuwashushia kipigo kisha kuwachoma moto hapo hapo huku mmoja kati ya hao watano akikatwa panga kwenye mguu na kudumbukizwa kwenye kisima na kufia humo humo.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Geita Dkt Adam Sijaona amekiri kupokea miili ya marehemu majira ya saa nane na nusu mchana wa leo walioletwa na gari la polisi ambao walifika muda mfupi baada ya tukio wakiwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio na kuwataja majina yao watu hao kuwa  ni Juma Patrick Kigara,Marwa Chacha Kigara,na wawili waliofahamika kwa Eze na Shija na wa tano akiwa hajafahamika jina lake.

Kamanda Paulo amesema tayari watu watatu akiwemo kiongozi wa jeshi la jadi sungusungu wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi huku jeshi likiendelea kufanya  uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi wa habari hizi kutoka mkoani Geita Valence Robert ni kwamba asilimia kubwa ya wanaumme wamekimbia miji yao kutokana na msako mkali unaofanywa na jeshi la polisi kubaini wahusika wa tukio hilo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post