TBS NA VITA DHIDI YA UUZAJI NGUO ZA NDANI ZA MITUMBAShirika la viwango nchini TBS limepiga marufuku uuzaji wa nguo za ndani za mitumba na atakayekamatwa akijihusisha na biashara hiyo hatua kali zaitachukuliwa dhidi yao

Hatua hiyo imekuja baada ya kugundulika nguo hizo zinaleta madhara makubwa kwa watumiaji

Kufuatia tamko hilo shirika hilo tayari limeshaanza zoezi la kuingia katika masoko ya jijini Dar es Salaam kukamata wafanyabiashara hao

Afisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile amesema wameamua kuingia katika masoko ili kuziondoa bidhaa kwani zinasababisha madhara kwa binadamu.

Amesema hatua hiyo imekuja kwa kuwa walitoa agizo miezi mitatu kabla kwa wafanyabiashara ili kuacha kuuza bidhaa hizo baada ya kubainika hazipo katika kiwango.

Amesema wameanza katika soko la Tandika na kufuatiwa na masoko mengine kwani bidhaa hizo hazitakiwi kuingia katika soko kwa mujibu wa sheria.

Zoezi hilo wamefanikiwa kuwakamata watu kadhaa huku wengine kukimbia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments