WANAWAKE WAONGOZA KWA VITAMBI ,UZITO ULIOKITHIRI NA KISUKARI SHINYANGA,FUATILIA STORI NA PICHA HAPA NI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI

Awali wapiga matarumbeta wakifanya yao leo kuanzia mida ya saa mbili asubuhi wakati wa maandamano ya kutembea kwa miguu kwa kasi yaliyoanzia katika hospitali ya mkoa wa shinyanga kupitia maeneo mbalimbali ya mjini Shinyanga  yakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga hadi katika viwanja vya shy-com ambako mgeni rasmi ,mkuu wa mkoa wa shinyanga alitoa hotuba yake kuhusu siku ya kisukari duniani kimkoa
Ni katika mitaa mbali mbali mjini Shinyanga maandamano/matembezi yakiendelea kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga ,katikali ni katibu tawala wa mkoa Dkt Anselim Tarimo kushoto ni mganga mkuu wa  mkoa wa shinyanga Dkt Ramadhan Kabala wakitembea kwa kasi kuhamasisha wananchi wafanye mazoezi kwa ajili ya afya zao
Wa pili mbele  mwenye jaketi ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Anna Rose Nyamubi akitembea wakati wa maandamano ya leo katika siku ya kisukari duniani ambapo kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na shirika la bima ya afya imebainika kuwa
wanawake katika mkoa huo wanaongoza kwa kuwa na uzito mkubwa ukilinganisha na wanaumme  lakini pia wanaongoza kwa kuwa na ugonjwa wa kisukari

Wanafunzi wa  shule za sekondari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika maadhimisho ambapo  kauli mbiu mwaka huu ni TUJIKINGE NA TUIJENGE JAMII IJAYO NA UGONJWA WA KISUKARI
Kikundi cha watafuta njia(Pathfinder club) kutoka kanisa la Waadventista Shinyanga wakimpokea mkuu wa mkoa katika viwanja vya Shy-com pamoja na kuonesha gwaride lao muda mchache baada ya matembezi kukamilika
maafisa wa ulinzi na usalama wakiwa katika eneo la viwanja vya shycom wakifuatilia mawili matatu yaliyokuwa yanajiri

Msafara wa maandamano ukiingia uwanjani,hao ni baadhi ya madaktari na wauguzi kutoka hospitali ya mkoa wa shinyanga wakihamasisha jamii kujenga tabia ya kufanya mazoezi

Mbele ni Kiongozi wa kikundi cha Watafuta njia akimwongoza mkuu wa mkoa kuelekea katika eneo la jukwaa kuu tayari kwa kutoa hotuba yake ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kuepuka tabia za kula kula ovyo

SIKU NZURI--mazoezi ndiyo  kila kitu furaha inakuja yenyewe
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akitoa hotuba ambapo
amewataka wananchi kuwa na nidhamu ya maisha kwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara  na kuepuka mitindo mibaya ya ulaji na unywaji na wajenge tabia ya kufanya mazoezi angalau muda wa nusu saa kila siku ili kuepuka kisukari na magonjwa mengine sugu kwani kiini chake kikuu ni uzito uliokithiri.
Tafiti zinaonesha kuwa 35.6% ya wananchi wa Shinyanga wana uzito mkubwa kuliko urefu wao,ambapo wanaumme ni 23% ya wanaumme wote,wanawake 52.4% ya wanawake wote wenye umri kati ya miaka 15 hadi 80

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Annarose Nyamubi akimkaribisha mkuu wa mkoa wa shinyanga ili azungumze na wakazi wa mkoa wa shinyanga.
baadhi ya alili za ugonjwa wa kisukari ni,kupungua nguvu za kiume, kukojoa sana mara kwa mara,kupata kiu kali na mara kwa mara,kujisikia njaa sana,uzito kupungua,kupunguza uwezo wa kuona,kutapika na kuumwa tumbo pamoja na miguu na mikono  kupata ganzi au kuwaka moto na kupoteza hali ya furaha
                                     
Awali mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ramadhan Kabala akizungumza katika viwanja vya Shy-com ambapo pamoja na mambo mengine amesema
22.9% ya watu wenye umri chini ya miaka 45 wana uzito mkubwa wakati wenye umri zaidi ya miaka 45 ni 12.8% ndiyo wenye uzito mkubwa huku asilimia 5.2 ya watu wa Shinyanga wana ugonjwa wa kisukari,ambapo wanaumme ni 4.5% ya wanaumme wote wakati wanawake ni 6.1% ya wanawake wote na kwamba 16.8% ya wananchi wa shinyanga wana uzito uliokithiri(viriba tumbo au vitambi),wanaumme ni 14.9 na wanawake ni 28%.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post