Noma Kweli---!!! WANAOKAMATA WACHAWI MAARUFU KAMCHAPE NAO WAKAMATWA MKOANI TABORA


Baadhi ya Wataalamu wa kufichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina na uchawi maarufu KAMCHAPE wamejikuta wakiwa kwenye mikono ya dola baada ya  kuendesha zoezi la kufichua uchawi katika nyumba kadhaa kwenye vijiji mbalimbali vya manispaa ya Tabora ambapo baadhi ya wananchi walililalamikia zoezi hilo kwa madai kwamba limekuwa likiwadharirisha baadhi ya watu pamoja na kujenga chuki ambazo huenda zikasababisha madhara makubwa katika jamii. Wataalamu hao tayari wameanza kufikishwa kituo kikubwa cha Polisi mjini Tabora kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya ambapo aliwataka kuacha mara moja zoezi hilo la kufichua wachawi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post