KIJANA AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO BAADA KUMCHOMA KISU MWENDESHA BAISKELI ILI AMWIBIE -SHINYANGA

NB-picha haihusiani na tukio


Kijana mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja jina wala makazi yake(28) ameuawa kwa kushambuliwa kwa kipigo kikali kisha kuchomwa moto baada kumchoma kisu tumboni mwendesha baiskeli maarufu daladala ili kumwibia baiskeli mwendesha baiskeli huyo.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika kitongoji cha Bubalaji kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga
ambapo walioshuhudia tukio wamesema marehemu alikuwa anafanya jaribio la kuiba baiskeli ya mwendesha daladala ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja.

Kufuatia kuchomwa kisu mwendesha baiskeli huyo alianza kupiga  kelele za kuomba msaada na muda mchache  watu waliokuwa jirani na eneo la tukio walikusanyika na kumkamata marehemu na kuanza kumshushia kipigo  na kisha kumchoma .

“Kijana huyo kabla ya kifo chake alimkodi mwendesha daladala aliyekuwa na baiskeli  katika eneo la Kambarage mjini Shinyanga ili ampeleke kijiji jirani cha Uzogore lakini walipofika katika mto uliopo eneo la kitongoji cha Bubalaji  kijana alimwamuru mwendesha daladala huyo asimame na baada ya  kusimama alimchoma  kisu tumboni na kutumia nafasi hiyo kuiba baiskeli yake",alieleza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mwendesha daladala anayesadikiwa kukodiwa na marehemu amekimbizwa  katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa matibabu baada ya kuchomwa kisu tumboni na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo
.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post