Mapenzi Noumaaa!!! JAMAA AUAWA KWA KUPIGWA GONGO KICHWANI BAADA YA KUFUMANIWA-KISHAPU

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina  la Masanja Joseph (44) mkazi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa gongo kichwani na Minas Mihangwa mkazi wa kijiji cha Seseko,kata ya Songwa,tarafa ya Mondo,wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amesema tukio hilo limetokea juzi saa tatu na nusu usiku katika kijiji cha Seseko kata ya Songwa tarafa ya Mondo wilayani Kishapu, baada ya marehemu kumfumaniwa na mke wa Minas Mihangwa.


Kamanda Kihenya amesema chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa kimapenzi na kwamba jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa wa mauaji hayo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post