HATARI!!--MWIZI WA PIKIPIKI AFUNGWA NA KUBURUZWA KWENYE PIKIPIKI KISHA KUCHOMWA MOTO


Wananchi wakishuhudia  mwili wa mtu aliyetuhumiwa kuiba pikipiki ukiteketea kwa moto


Polisi wakiondoka na mwili wa marehemu
MTU mmoja asiyefahamika jina wala makazi yake, amepoteza maisha baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi ambao wameamua kujichukulia sheria mkononi.
Wananchi hao ambao ni wakazi wa eneo la Mtakuja Mbalizi, walifanya tukio hilo jana majira ya saa mbili asubuhi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtakuja Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye Masinga, alisema kuwa  marehemu huyo alidaiwa kuiba pikipiki  eneo la Utengule.
Alisema, baadhi ya madereva wa bodaboda(pikipiki) walianzisha msako na kufanikiwa kumtia nguvuni marehemu huyo na kuanza kumshushia kipigo huku mwili wake ukiwa umefungwa kwenye pikipiki na kuuburuza barabarani umbali wa kilomita moja.
Alisema, mwili huo uliburuzwa na kufikishwa kwenye eneo la mlima reli maarufu kwa jina la eneo la adhabu kwa wahalifu  na kuchoma moto mwili wake.
Aidha, katika tukio hilo fundi ujenzi aliyekuwa katika eneo hilo Asangalwisye Mayasu(50) mkazi wa kivukoni, alijikuta akiambulia kipigo baada ya kujaribu kuwazuia wananchi ambao waliamua kujichukulia sheria mkononi.
“Baada ya msamalia huyu kupigwa na kuumizwa vibaya serikali ya kijiji ilimkimbiza hospitali Teule ya ifisi na kwamba hali ya afya yake si nzuri hali iliyopelekea mke wake aitwaye Kristina Kyando (45) Kuzirai,”alisema.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi litahakikisha linawatia mbaroni watu wote waliohusika na mauaji hayo.
Kumeibuka kwa vitendo vya madereva  pikipiki kujichukulia sheria mkononi ambapo hivi karibuni walifunga barabara ya Iwambi Jijini Mbeya kwa kulishinikiza jeshi la polisi kuwaachia watuhumiwa wawili ambao  walituhumiwa kuiba pikipiki ili wawaue.
CHANZO-Utamu specially

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post