|
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Bi Anna Rose Nyamubi akitoa hotuba ya ufunguzi katika mkutano wa taftishi kuhusu maombi ya Shirika la umeme nchini TANESCO kurekebisha bei za huduma za umeme,mkutano ambao umefanyika katika ukumbi wa Green View ,Kambarage mjini Shinyanga,Wakati wa kutoa maoni yake kuhusu ombi hilo la Tanesco mkuu huyo wa wilaya alitoa ushauri kwa shirika hilo kutoharakisha mchakato huo kutoka kuongeza bei ya umeme kutoka shilingi 197.81 kwa uniti moja
hadi shilingi 332.06 ikiwa ni ongezeko la shilingi asilimia 67.87.Amesema gharama hiyo ni kubwa ukilinganisha na maisha ya wananchi lakini pia akapendekeza shirika hilo litoe elimu zaidi kwa wananchi kuhusu ombi lao |
|
Mwakilishi wa
mkurugenzi mtendaji mkuu wa shirika hilo bwana Godwin Ngwilimi akitoa taarifa juu ya ombi la TANESCO kuongeza bei ya umeme nchini ambapo alisema pamoja na kupitia katika changamoto nyingi lakini serikali bado inaendelea kuwasaidia,na kupitia mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa watahakikisha kuwa watanzania wengi zaidi watapata umeme hadi vijijini.Alisema lengo la kupandisha bei hiyo ya umeme ni
kuliwezesha shirika hilo kukabiliana na ongezeko la gharama za uendeshaji |
|
Mmoja wa wananchi katika mkutano huo wa kutoa maoni,bi Elisiana akizungumza ambapo alisema hakubaliani na ombi la TANESCO kwani shirika hilo bado halijaboresha huduma zake na kwamba wengi wa wafanyakazi wake wanapata mishahara mikubwa hivyo ni bora waangalie wapunguze,lakini pia bado gharama za huduma ni kubwa,umeme unakatikakatika,nguzo mbovu nk |
|
Mwandishi wa gazeti la Nipashe Marco Maduhu akichukua mawili matatu kuhusu maoni ya wadau wa umeme katika mkutano huo,pembeni ni Bi Suzy Butondo wa gazeti la Mwananchi na The Citizen |
|
Maafisa wa TANESCO wakichukua maoni ya wananchi,kushoto ni meneja wa TANESCO mkoa wa Shinyanga Gamba Maugira |
|
Maafisa wa baraza la ushauri la watumiaji huduma zinazodhibitiwa na EWURA(EWURA CCC) na baraza la ushauri la serikali wakati wa mkutano huo leo wakifuatilia maoni ya wawakilishi wananchi zaidi ya wakazi zaidi ya elfu 61 wa manispaa ya shinyanga ambapo asilimia kubwa ya waliotoa maoni hawakubaliana na ombi la TANESCO la kongezaa bei ya huduma. |
|
Wadau wa umeme katika mkutano |
|
Wengi wa watoa maoni pia walitoa kero zao kama vile wateja kukalishwa kwenye foleni kwa muda mrefu wanapokwenda kulipia bili za umeme,kukadiriwa bili,kukerwa na tabia ya baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco wasio waaminifu wanaoshirikiana na wateja kuiba umeme |
|
Aliyesimama ni Mwakilishi wa mkuu wa EWURA Injinia Anastas Mbawala akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema mkutano huo ni sehemu ya uchunguzi unaofanywa na EWURA kupata maoni ya wadau wa huduma ya umeme kabla ya kutoa uamuzi kuhusu maombi yaliyowasilishwa na TANESCO ya kurekebisha bei |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553