SUNGUSUNGU WACHANGIA MADAWATI BUBALE - SHINYANGA

 Awali mbunge wa jimbo la solwa Mheshimiwa Ahmed Ali Salum akiwasili katika eneo la kikao cha kukabidhi madawati kwa uongozi wa shule ya msingi Bubale iliyopo kata ya Masengwa wilaya ya Shinyanga,alivaa kofia ndiyo mbunge wa solwa akishikana mkono na Mkurugenzi wa wilaya ya shinyanga Mohammed Kiyungi .


Jeshi la sungusungu la kijiji cha Bubale ambalo limeshiriki katika kuchangia madawati 77 yenye thamani ya shilingi milioni 5 na laki 5 kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ambao wamekuwa wakikaa chini kwa muda mrefu. Hapa wanatoa burudani kwa mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa solwa

                                     

Mbunge wa solwa Ahmed Salum,aliyevaa kofia, hapa mzuka umepanda na akaamua kuungana na jeshi la sungusungu kutoa burudani wakati wa kukabidhi madawati 77 ikiwa ni mchango wa jeshi hilo kwa kushurikiana na wananzengo wa kijiji hicho cha bubale kilichopo katika kata ya masengwa.Lakini mwenye Suti nyeusi ni diwani wa kata hiyo Nicodemus Luhende akiwa na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya shinyanga wakitoa wakionesha furaha yao
                        

Mwalimu mkuu wa shule hiyo  Eliakim Mathew akizungumza wakati wa kukabidhiwa madawati hayo ambapo alisema shule yake ina wanafunzi 653 na walimu 14

Wanafunzi wa shule hiyo wakisoma shairi ambapo walieleza kufurahia kitendo cha wazazi wao kuwapatia madawati

SAFI SANA NDUGU YANGU ....Mbunge wa solwa na diwani wa masengwa wanakaa katika moja ya madawati yaliyokabidhiwa

 Kushoto ni mwandishi wa radio faraja Geni Elias akichukua mawili matatu katika kikao hicho,kushoto ni mwalimu mkuu wa shule bubale
Afisa mtendaji wa kijiji cha Bubale,Frank Naiso akisoma risala kwa mgeni rasmi ambapo alisema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo ukosefu wa barabara,tatizo la maji  ambapo wameomba mchakato wa maji ya kutoka ziwa victoria ufike mapema katika kijiji hicho kwani hivi sasa wanatembea zaidi ya kilomita 6 kutafuta maji,igawa hata hivyo mbunge wao alisema wananchi watapata maji hayo hivi karibuni

Wananchi wanafuatilia kinachoendelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post