MZEE AJINYONGA KWENYE SHAMBA LA MAPERAKaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya


Mkazi wa kitongoji cha Mwankumbo kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi  tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga Shija Mfuko Jondo(57) amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba ya katani juu ya mti wa mwembe katika shamba la mapera katika eneo la Nhumbili lililopo kata ya Tinde wilaya ya shinyanga

Mtoto wa marehemu aitwaye Shija Mathias ameiambia malunde1.blogspot.com kuwa baba yake alikuwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo mwezi Juni mwaka huu,na tayari alikuwa akifanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya yake ila siku hiyo aliaaga asubuhi kuwa anakwenda kufanya mazoezi na hakurudi.

Alisema walimkuta mzee huyo amejinyonga kwenye shamba la mapera hapo juzi jioni

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo chake bado hakijafahamika ingawa marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments