JAJI FRANCIS MUTUNGI ATEULIWA KUWA MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA...AVAA KIATU CHA TENDWA

P 1
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mh. Francis Mutungi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha majaji 10, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mwaka jana. (Picha na  MOBLOG MAKTABA)
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.


 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post