MTOTO ABAKWA NA KUTOBOLEWA MACHO-SHINYANGA


Na Marco Maduhu


Mtoto mmoja  wa kike mwenye umri wa miaka 7  jina lake linahifadhiwa ambaye ni mkazi wa Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga amefanyiwa ukatili wa ,kijinsia kwa kuingiliwa kinyume na maumbile na kisha kutobolewa jicho la kulia na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Machi 26 mwaka huu.

Mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dr, Giliadi Kasoga alikiri kumpokea mtoto huyo majira ya saa nane usiku  kwa ajili ya matibabu.

"Nime mpokea mtoto huyo majira ya saa nane usiku, huku akiwa hoi na baada ya kuanza kumfanyia vipimo na ndipo nilipobaini kuwa alifanyiwa kitendo hicho kinyume na maumbile ambapo nilikuta michubuko na baadhi ya manii"alisema Dr kasonga

 Dr.Kasoga aliendelea kusema kuwa mtoto huyo alifikishwa  hospitalini hapo na jeshi la  sungusungu ambao walisema kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa ametelekezwa katika eneo moja hatarishi huko Kizumbi mara baada ya kufanyiwa ukatili huo wakati wakiwa katika doria ya usiku.

Kufuatia hali ya mtoto huyo kutokuwa ya kuridhisha na ndipo walipo amua kumpatia Rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando  jijini Mwanza kwa matibabu zaidi kutokana na upungufu wa vifaa vya kitaalamu katika hospitali hiyo ya mkoa wa shinyanga

Kwa upande wao baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi wanaochunguza chanzo cha tukio hilo walisema kuwa taarifa kamili zitatolewa kupitia kwa kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa wa shinyanga ACP Evarist Mangala mara baada ya uchunguzi wa tukio hilo utakapo kamilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post