UKATILI WA KUTISHA -IRINGA


Kijana  huyo akiwa  hoi kwa  kipigo baada ya  kutupwa  porini
Askari  polisi  wakimsaidia  kijana  huyo ambae alikuwa hajitambui
WAKATI leo ni kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani, mkazi mmoja wa ndiuka katika Manispaa ya Iringa ambae jina lake  bado kufahamika  amenusurika  kifo kwa  kupigwa na   kundi la  watu  wanaojiita kuwa na asila kali  wakazi  wa Ndiuka akidaiwa ni kibaka japo habari za  nyuma ya pazia zikidai kuwa ni kutokana na wivu wa kimapenzi
Mmoja kati ya mashuhuda  wa tukio  hilo ameueleza mtandao huu kuwa  kijana  huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke  mmoja wa eneo  hilo la ndiuka na baada ya  kumtosa ndipo mwanamke huyo alipopiga kelele za mwizi na kupelekea  wananchi kumpa kipigo na kumtupa katika korongo kwenye mlima wa Ipogolo mjini Iringa.

Hata  hivyo jitihada za wasamaria  wema  kuoka maisha yake  zilifanyika kwa  kupiga  simu polisi na polisi  kufika eneo hilo  kumuokoa kijana  huyo akiwa hajitambui  .
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post