MTOTO AZALIWA UTUMBO UKIWA NJE YA TUMBO-SHINYANGA



Na Marco Maduhu

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aitwaye Elizabeth George mkazi wa Bubale katika wilaya ya Shinyanga Vijijini amejifungua mtoto wa kike, huku utumbo wake ukiwa nje ya tumbo.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga Dr Fredrick Mlekwa amesema mwanamke huyo amepokelewa hospitalini hapo majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo, huku akiwa anaumwa uchungu, ambapo alijifungua mtoto huyo majira ya saa saba usiku.

Akielezea hali hiyo kitaalam amesema inatokana na kasoro za maumbile au upungufu wa vimelea vya vitamin kwa mama mzazi wa mtoto huyo na kwamba wanawake wajawazito wanapaswa kuhudhuria kliniki mapema, ili wataalam waweze kubaini matatizo ya namna hiyo kabla ya kusababisha madhara zaidi.

Hata hivyo Dr Mlekwa amesema wamelazimika kumpa rufaa mwanamke huyo ya kwenda katika hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza, kutokana na hospitali ya mkoa wa Shinyanga kutokuwa na wataalamu, ikiwemo vifaa vya kusaidia kumhudumia mtoto huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments