AFARIKI AKITOA MIMBA KAHAMA- SHINYANGA




Mwanamke mmoja aitwaye Asha Damanya (36) mkazi wa  kijiji cha Mwamala wilyani Nzega mkoani Tabora amefariki dunia wakati akitoa mimba katika Zahanati ya Matina iliyopo katika kata ya Nyahanga Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 Walioshuhudia tukio hilo wamesema mwanamke huyo alifarika dunia Desemba 19 mwaka huu majira ya saa 12 jioni wakati akitoa mimba katika zahanati hiyo.

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo Kaimu Kamanda wa polisi  wa jeshi hilo SSP Onesmo Lyanga amesema tayari wanamshikilia mganga wa zahanati hiyo Damas Matina (63) kwa mahojiano zaidi ,huku akiwaasa wananchi kuacha tabia ya kutoa mimba kwani ni kosa la jinai na ni hatari kwa maisha ya mwanadamu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments