polisi wakiwasaka vijana walioeneza uvumi wa kuwepo kwa msukule eneo la Mwangata mjini Iringa sasa
wananchi wakiwa wamesitisha shughuli zao kutaka kuona msukule unaodaiwa kuonekana
Polisi wakiwa katika msako wa kuwasaka wazushi wa taarifa hiyo ya kuonekana mtoto anayedaiwa kufa siku nyingi a.k.a Msukule
Polisi wakiwa katika msako eneo la Mwangata
Zimezuka
habari zenye utata ambapo inasemekana kuwa kuna
mtoto anayedaiwa kufa na kuzikwa kuonekana leo akidaiwa kuwekwa Msukule
.
Tukio
hilo limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa na kupelekea polisi
kufika kuwatawanya wananchi hao na kuwasaka wale ambao wanadaiwa
kueneza uvumi huo.
Hata
hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya waliokuwepo hapo ambaye
amethibitisha kuona msukule huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia .
Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule huyo.
Rai
ya mtandao huu kwa jamii ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla
kuepuka kuamini imani za kishirikina ambazo zinaweza kuvuruga amani
yetu.
PICHA ZOTE FRANCIS GODWIN