MME AUA MKE KWA FIMBO-SHINYANGA


Mwanamke mmoja aitwaye Munde Lunyiliga (30) mkazi  wa Kitongoji cha Mbapa Kijiji cha Busili Kata ya Bulyanhulu wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mme wake kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea Novemba 26 saa 11 alfajiri  mwaka huu,ambapo Mashaka Karuka (40) alimuua mke wake kwa kumpiga fimbo na kisha kukimbia baada ya tukio hilo.

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kamanda wa jeshi hilo ACP Evarist Mangalla amesema bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa bado zinaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments