MAZISHI YA SHARO MILIONEA ,KING MAJUTO AZIDIWA


Jeneza  lenye  mwili wa Sharo Milionea  likitolewa
Wananchi  wakiwa na huzuni wakati  mwili wa Sharo Milionea  ukitolewa
Umati  wa  waombolezaji  wakiwa nyumbani kwa Sharo Milionea


Shekh akiombea  mwili  wa jeneza  leye mwili wa Sharo Milionea

Waumini wa dini ya kiislamu  mkoani Tanga  wakiufanyia  dua za mwisho mwili wa Sharo Milionea
 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
Hapa  ndipo  mwili wa Sharo Milionea  ulipohifadhiwa
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.



Mamia ya  wakazi  wa mkoa  wa Tanga pamoja na  wasanii wa  kundi la Bongo Movie   leo  wameshiriki  kikamilifu katika mazishi ya msanii Sharo Milione yaliyofanyika  wilayani Muheza mkoani Tanga  umbali wa takribani kilometa 2 kutoka nyumbani  kwa msanii  huyo huku  vurugu  za hapa na pale  zikitokea  wakati wa kuanga mwili  huo

Wakati  mwili  wa msanii  Sharo Milionea  unaelekea  kuzikwa  hivi sasa  zimeripotiwa vurugu  kubwa  kutokea wakati  wa  mazishi ya msanii  wakati  wa shughuli ya  kuaga mwili  huyo.
Imedaiwa  kuwa   umati  mkubwa  wa  wananchi  wamepata  kujitokeza kwa wingi  kuaga mwili  wa msanii  huyo  huku  baadhi  wakigombea  kuaga mwili  huo .
Mwandishi  wa  mtandao  huo ambae  anaendelea  kuripoti moja  kwa  moja (LIVE)  kupitia  kituo cha  radio  Nuru Fm  pia  amesema  kuwa  kwa sasa  mwili  wa Sharo Milionea  unatolewa  nyumbani kwenda  katika makaburi  yaliyoandaliwa 

Hata  hivyo  vurugu hizo  zinadaiwa  kutokea  wakati  wa  kuaga na  kila mmoja akitaka  kuugusa  mwili  wa Sharo Milionea .

Miongoni  mwa  viongozi  wa  vyama  vya  siasa  waliofika  ni pamoja na  Nappe Nauye ,Mukama  huku Miongoni  mwa  wasanii  waliofika hapo wa  kundi la Bongo Movie ni pamoja na Ray , Kitale na  wengine  na   kuwa mwili  huo  umezikwa  eneo la umbali  wa kilomita  2  kutoka  nyumbani kwa marehemu .
 
SOURCE:Francisgodwinblog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments