HATARI:WATU WANNE WAUAWA,WATATU KWA KUKATWAKATWA MAPANGA,MMOJA KWA MAWE NA FIMBO-SHINYANGA.

Na Malunde Kadama

Watu wane wameuwa katika nyakati totafuti mkoani Shinyanga,watatu kati yao kwa kukatwa na mapanga na mmoja kushambuliwa kwa mawe na fimbo na wananchi wenye hasira kali .
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla amesema Novemba 27 majira ya saa 3 usiku mwanamke mmoja aitwaye Mhoja Mathias (47) mkazi wa kijiji cha Ibingo kata ya Samuye katika wilaya ya Shinynga vijijini akiwa amelala na mme wake Mtugwa Mayanga (78) aliuawa kwa kukatwa mapanga kichwani,kisogoni na mabegani na watu wasiojulikana,na kusababisha kifo chake papo hapo, huku mme wake akiwa ametolewa nje mbali na  nyumba yake na kisha kumtelekeza huko.
Amesema siku hiyo hiyo na muda kama huo, huko katika kijiji cha Mwasegaki kata ya Solwa tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini mwanamme mmoja aitwaye Hoja Lusheshanija(35) na mke wake Christina Stephano(29) wakiwa nyumbani kwao waliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga sehemu za shingoni na mikononi na watu wasiofahamika.
Tayari jeshi la polisi linawashikilia watu watatu watiliwa mashaka, kuhusiana na tukio  hilo,ambao na Shija Magutabeli,Nkwabi Isheshameja na Marco Manyandodi.
Aidha ameongeza kuwa  huko katika kitongoji cha Igomelo,kata ya Mhongolo wilayani Kahama mwanamme asiyejulianana jina wala makazi yake ,umri 25-30 alishambuliwa kwa mawe na fimbo na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na kusababisha kifo chake papo hapo, jana majira  ya saa moja asubuhi.
Kamanda huyo wa polisi amesema vyanzo vya mauaji yote havijulikani,ambapo uchunguzi bado unaendelea na juhudi za kuwatafuta wahusika zinaendelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments