 |
Askari wakitazama Helment ya dereva boda boda iliyokuwa imeweka juu ya miti |
 |
mwili wa Dereva boda boda Abeli Nyunza aliyeuwawa ukiwa umetupwa katika korongo juu ni dimbwi la damu |
 |
Polisi wakiwa eneo la tukio |
 |
Watu
wanaosadikika kuwa ni vibaka wamemuua kwa kumpiga na kitu kizito
katika paji la uso dereva boda boda eneo la National mjini Iringa Abeli
Nyunza na kumpora piki piki yake.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Muungano
Frelimo mjini Iringa jirani na shule ya msingi Muungano.
Wakielezea
juu ya tukio hilo mashuhuda waliozungumza na mtandao huu wamedai
kuwa majira ya usiku walisikia mlio wa pikipiki na ghafla ulizimika
na baada ya hapo ilisikika sauti ikiita kwa nguvu Peter ! Peter !
mfano wa mtu aliyekuwa akiomba msaada na baada ya dakika kama 10
hivi ukimya ulitanda na ghafla ulisikika mlio wa pikipiki ukiondoka
kwa kasi.
Mwenyekiti
wa boda boda mjini Iringa Macurius Chengulla mbali ya
kuthibitisha kifo cha dereva boda boda mwenzao huyo bado amesema
kuwa wameweka mkakati wa kuendesha msako ili kuwabana wahusika wa
mauwaji hayo.
Chengulla
amesema kuwa matukio hayo ya kuuwawa kwa madereva boda boda kwa
Manispa ya Iringa ni tukio la kwanza kwa mwaka huu japo matukio ya
kutekwa na kujeruhiwa yamekuwa yakitokea .
Habari na Francis Godwin |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment