HATARI:MWANAMKE ATUMBUKIA CHOONI WAKATI AKIFANYA MAPENZI NA HAWALA, HUKU MUMEWE AKIWA MAUTUTI CHUMBANI


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la TIENA MWAZEMBE mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji Hangomba kata ya Bara wilayani Mbozi mkoani Mbeya amenusurika kufa baada ya kutumbukia chooni wakati akifanya mapenzi huku mumewe akiwa maututi chumban


Habari za uhakika kutoka kijijini hapo zinadai kuwa mwanamke huyo licha ya kuwa mke wa mtu alikuwa anafanya ngono chooni na WASI MGALA wakati mumewe akiwa ndani anaumwa na kwamba alidumbukia choo baada ya banzi alilokuwa amekanyaga kukatika wakati wanafanya tendo hilo.


Mwanamke huyo alidumbikia kwenye choo chenye urefu wa futi 17 na kwamba baada ya kudumbukia, mwanaume aliyekuwa naye chooni wakifanya ngono alikimbia na kumwacha mwanamke huyo akipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walifika na kufanikiwa kumtoa ndani ya shimo na kukimbiza kwenye duka la madawa linalomilikiwa na muuguzi LEONARD NZOWA ambaye alitoa huduma ya kwanza kabla ya kumfikisha katika hospitali ya Mbozi Mission.


Hata hivyo mume wa mwanamke huyo SAIKI GODFREY KAROTI amesema kitendo kilichofanywa na mkewe ni cha udhalilishaji na si cha uungwana.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post