Wananchi wa Kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga kesho watapiga kura kumchagua Diwani mpya ,kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Charles Magina aliyefariki dunia mwaka jana.
Uchaguzi huo unafanyika huku kukiwa kumeripotiwa vurugu kadhaa za kisiasa kati ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na wale wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambazo zimesababisha kujeruhiwa vibaya kwa mtu mmoja kwa kuchomwa mkuki tumboni.
Post a Comment