Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI ZAIDI YA 19,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA SH BILIONI 5.5 MADABA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Mtyangimbole katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba baada ya kukagua mradi wa maji 

Na Regina Ndumbaro, Ruvuma

Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekagua utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Mtyangimbole katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma, unaolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa vijijini.

Mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, kwa lengo la kupunguza adha ya kutafuta maji na kuboresha afya pamoja na ustawi wa jamii.

Mradi wa Maji wa Mtyangimbole unaogharimu shilingi bilioni 5.5, umesanifiwa kuhudumia mahitaji ya wananchi kwa kipindi cha miaka 20 na unatarajiwa kunufaisha jumla ya wananchi 19,316 kutoka vijiji vya Likarangilo, Luhimba na Mtyangimbole.

Kwa sasa, vijiji hivyo vitatu vina jumla ya wananchi 14,084 ambao wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo mara baada ya mradi kukamilika na kuanza kutoa huduma, huku uwekezaji huo ukitarajiwa kuimarisha upatikanaji wa maji kwa mahitaji mbalimbali ya kila siku.

Utekelezaji wa mradi huo ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma ya maji vijijini, kupunguza changamoto za upatikanaji wa rasilimali hiyo muhimu na kuboresha maisha ya wananchi, sambamba na kuchochea shughuli za kiuchumi kupitia upatikanaji wa maji safi na salama.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com