Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba, akitoa elimu ya ujasiriamali na fursa za kibiashara zinazopatikana mgodini kwa wananchi na wajasiriamali wa Kitongoji cha Mwingiro, Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba, akitoa elimu ya ujasiriamali na fursa za kibiashara zinazopatikana mgodini kwa wananchi na wajasiriamali wa Kitongoji cha Mwingiro, Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba, akitoa elimu ya ujasiriamali na fursa za kibiashara zinazopatikana mgodini kwa wananchi na wajasiriamali wa Kitongoji cha Mwingiro, Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Wakili Ambakisye Osiah, akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali na utambuzi wa fursa za kibiashara zinazopatikana katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Samwel Morango, akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali na utambuzi wa fursa za kibiashara zinazopatikana katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, wilayani Nyang’hwale mkoani Geita.

Sehemu ya wananchi na wajasiriamali wa Kitongoji cha Mwingiro, Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali na utambuzi wa fursa za kibiashara zinazopatikana katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
***
#Lengo ni kupanua wigo wa watanzania kushiriki kwenye fursa za biashara, ajira.
Katika kufanikisha dhamira yake ya kuwezesha wananchi wanaoishi jirani na mgodi wa Bulyanhulu wananufaika, Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale imetoa mafunzo ya ujasiriamali na utambuzi wa fursa za kibiashara zilizopo mgodini kwa wananchi wa kitongoji cha Mwingiro kilichopo Nyang’hwale mkoani Geita.
Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Afisa Uhusiano kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Mary Lupamba, yamelenga kuwajengea uwezo wananchi ili waweze kutambua mahitaji ya mgodi, kuandaa na kuwasilisha zabuni kwa usahihi, pamoja na kuongeza uwezo wao wa kushiriki katika fursa za biashara zinazotolewa na Mgodi.
Katika mafunzo hayo,Mary Lupamba aliwaeleza jinsi mgodi unavyotekeleza sera ya ushirikishwaji wazawa katika mnyororo wa biashara ya madini (Local Content) na kuwataka wananchi, wajasiriamali, vijana, na wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu ambao upo chini ya kampuni ya Barrick inayoendesha shughuli zake kwa ubia nchini kupitia kampuni ya Twiga.
Kwa Upande wake Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Wakili Ambakisye Osiah, amesema utekelezaji wa sheria ya Local Content umeondoa malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kutoshirikishwa katika shughuli za madini na sasa unaleta manufaa ya moja kwa moja kwa jamii zinazozunguka migodi.
Ambakisye pia alitumia fursa hiyo kwa kutoa rai pia kwa wafanyabiashara kutumia mfumo wa Ununuzi wa Umma ili waweze kupata taarifa na kushiriki katika zabuni mbalimbali za Serikali ili kuongeza ushiriki wa wazawa katika fursa za kiuchumi.
Baadhi ya Wananchi walioshiriki katika mafunzo hayo wameishukuru Serikali ya Wilaya ya Nyang’hwale kwa kuweza kuwakutanisha na wadau kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na wameweza kuelewa jinsi ya kufanya biashara na mgodi kupitia sera ya uwezeshaji wazawa katika sekta ya madini (Local Content), hatua inayozidi kufungua milango ya kiuchumi kupitia ajira, kandarasi za usambazaji bidhaa na huduma mbalimbali kwenye migodi mikubwa.
Mbali na mafunzo haya Barrick imekuwa ikiwajengea uwezo wafanyabiashara wa ndani kupitia Programu yake ya kuendeleza biashara za ndani ili ziweze kunufaika na sekta ya madini ijulikanayo kama Local Business Development Programme (LBDP) ambapo wajasiriamali kutoka wilaya za Msalala, Kahama na Nyang’hwale wamenufaika na mafunzo hayo.
Katika program hiyo wajasiriamali waliopo maeneo yanayozunguka mgodi wa Barrick Bulyanhulu yamekuwa wakipatiwa elimu ya utambuzi wa kuchangamkia fursa za kibiashara na kunufaika na uwekezaji wa mgodi huo sambamba na kupata maarifa zaidi ya kuendesha biashara zao kitaalamu.
Barrick inaendeleza dhamira yake ya kuendelea kutekeleza sera ya ushirikishwaji Watanzania katika sekta ya Madini (Local Content) kwa ufanisi ili sekta hii inufaishe Watanzania wengi zaidi kutokana na uwekezaji wake kwa kuwa migodi ya Twiga- Barrick inazo fursa nyingi kwa ajili ya watanzania wazawa ili waweze kushiriki kwenye sekta ya madini.
Kutokana na utekelezaji wa sera hii kwa vitendo, migodi ya Barrick -Twiga ya North Mara na Bulyanhulu inashikilia rekodi ya kutunukiwa tuzo kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kutokana na kutambua mchango wake.
Sera na kanuni za maudhui ya ndani (Local Content) nchini zinalenga kuhakikisha kuwa rasilimali na miradi ya uwekezaji hasa katika sekta ya madini, nishati, na uchumi wa kidijitali zinawanufaisha watanzania kwa kuwakutanisha na fursa za ajira, manunuzi, na uhamisho wa teknolojia ili kupanua wigo wa ushiriki wao kwenye sekta hizo hususani ya madini.
Akiwa mgeni rasmi wa Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji Watanzania katika sekta ya madini, Waziri wa Madini , Anthony Mavunde ambayo ilikuwa na kauli mbiu ‘ongezeko la ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya Madini, chachu ya ukuaji wa uchumi Tanzania jijini Mwanza karibuni, Mavunde Mavunde alisema kwamba sekta ya madini imeweza kuchangia 10.0 % ya Pato la Taifa (GDP) na mafanikio hayo yanatokana na utekelezaji mzuri wa Maudhui ya Ndani (Local Content).
“Mafanikio katika sekta ya madini ni makubwa na mpaka sasa ninavyozungumza sekta hii ya madini imechangia Tsh 985 billioni kwenye mfuko mkuu wa serikali haya ni mafanikio makubwa sana kwenye sekta ya madini,” alisema Mavunde.
“Sekta hii ya madini inakua kwa kasi kubwa pamoja na mambo mengine kuna viwanda tisa vinajengwa vya kuchakata na kusafisha dhahabu ili kukuza mnyororo wa dhamani,” aliongeza Waziri Mavunde.
Waziri Mavunde alisema kwamba katika utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini kupitia kanuni ya maudhui ya ndani (Local content) kuna watanzania 16,874 ambao wameajiriwa kwenye sekta ya madini hapa nchini.
Sehemu ya wananchi na wajasiriamali wa Kitongoji cha Mwingiro, Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali na utambuzi wa fursa za kibiashara zinazopatikana katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.









TAFUTA HABARI
Social Plugin