Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma
Katibu wa Wizara ya Utamaduni , Vijana na Michezo wa Burundi, Bw. Riziki Jackob
NA. ELISANTE KINDULU, ZANZIBAR
MAKAMU wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wadau wa kiswahili kuhakikisha wanatoa huduma bora ya kazi za kiswahili ili kukidhi mahitaji ya wateja wake.
Akimwamkilisha Makamu wa pili wa Rais ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano la 10 la kiswahili lililoandaliwa na Baraza la kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) jana katika ukumbi wa chuo cha polisi Ziwani, Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma alisema ili kazi zinazoendana na utamaduni wa Kiswahili ziwe bora hakuna budi wanaoandaa kazi hizo wazifanye kwa ufanisi mkubwa.
Mhe.Waziri alisema kuwa kiswahili kina manufaa makubwa kama kikitumiwa kwa weledi na kufanya kuwa fursa.
Mhe. Waziri alitaja kazi za kiswahili zinazoweza kutengenez kipato kwa wataalam wa lugha hiyo ikiwa ni pamoja na uandishi wa vitabu, makala na majarida, Sanaa za maonyesho, ufasiri na ukalimani pamoja kufundisha k
Kiswahili kwa wageni.
Mhe. Waziri huyo alishauri taarifa zote za kongamano ikiwemo mafanikio na changamoto zinazojadiliwa kwenye kongamao ziripotiwe kwenye mamlaka na wizara husika kwaajili ya utekelezaji zaidi.
Aidha Mhe. Waziri Pembe aliwataka wadau wa kiswahili na taasisi mbalimbali kuwapa maua yao wabobezi mbalimbali wanaoiletea sifa nchi badala ya kusubiri mpaka wakati wa mauti yao.









TAFUTA HABARI
Social Plugin