Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AFUNGWA MAISHA JELA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 9


Na COSTANTINE MATHIAS, Maswa

‎
‎MAHAKAMA ya Hakimu Mwandamizi wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha kwenda jela Maisha, Jilala Kondela (64), Msukuma, mkulima, mpagani na mkazi wa Kijiji cha Dulumwa wilayani humo kwa makosa mawili ya kubaka.

‎
‎Katika hukumu ya shauri la jinai Na.15102/2026 imesomwa leo 12/11/2026 katika Mahakama ya wilaya ya Maswa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Nhandala Kondela, ambapo Mshatakiwa alishtakiwa kwa Makosa Mawili yote yakiwa ni Kubaka kinyume na vifungu vya 130(1)(2) (e) na 131(3) vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2023.

‎
‎Awali Mahakamani hapo , ilidaiwa na upande Jamhuri ambao uliwakilishwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Mkaguzi wa Polisi Vedastus Wajanga, kuwa Mnamo tarehe tofauti mwezi January Mwaka 2026 na tarehe 13 mwezi February 2026 katika Kijiji cha Dulumwa Mshatakiwa alimbaka Muhanga jina limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 09.

‎
‎Na tarehe 17/06/2026 Mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa kituo Cha Polisi Maswa na alipohojiwa alikana kutenda kutenda kosa hilo, Na baada ya upelelezi kukamilika Mshatakiwa tarehe 06/07/2026 alifikishwa mahakamani na kusomewa Makosa yake ambapo alikana kutenda makosa hayo.

‎
‎Jumla ya mashahidi wanne walitoa ushahidi wao ukiwemo ushahidi wa Muhanga ambae alithibisha kubakwa zaidi ya mara moja na mshtakiwa pindi ambapo walezi wake walipokuwa shambani kwa shughuli za kilimo.


‎Katika utetezi wa mshtakiwa ambae alijitetea yeye mwenyewe bila kuwa na shahidi mwingine alidai kuwa yeye hajambaka muhanga bali ni chuki zinazotokana na umiliki wa maeneo lakini alipoulizwa kuhusiana na huo utetezi na Jamhuri alishindwa kuleta ushahidi au uthibisho wa huo utetezi wake.

‎
‎Alipopewa nafasi ya maombolezo, aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwakuwa yeye ni Mzee wa umri wa miaka 64, hivyo kutokana na umri wake anaomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu ni kosa lake la mara ya kwanza.

‎
‎Upande wa Mashtaka uliomba Mshtakiwa apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na onyo kwa wengine wenye nia au lengo la kufanya kitendo alichokifanya mashtakiwa, ukizingatia kuwa vitendo vya Ubakaji vinaongeza ndani ya jamii na athari zake haziwezi kusahulika kwa Mtendewa na ukizingatia kuwa muhanga ni mtoto mwenye umri wa miaka tisa na ndio nguvu kazi kwa Taifa la kesho.

‎
‎Mahakama ya wilaya ya Maswa ilimtia hatiani Mshitakiwa kwa Makosa yote mawili Jilala Busanda.

‎
‎Ndipo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya wilaya ya Maswa Nhandala Kondela alimhukumu Mshitakiwa Jilala Busanda adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kila kosa pamoja na fidia kwa muhanga kiasi cha shilingi 700,000/= na kifungo hicho atatumikia kwa pamoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com