Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi (wa pili kutoka kushoto), Katibu Tawala wilayani humo Fatma Mohamed (wa kwanza kushoto), Mkuu wa TAKUKURU wilayani humo Atuganile Stephen (aliyevaa koti jekundu) na wapili kutoka kushoto Mhe. Lwinzi Kidiga anayekabaidhiwa tuzo kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na RUSHWA wilayan humo Septemba 23,2026
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, imemkabidhi tuzo aliyekuwa Diwani wa Kata ya Maganzo, Mhe. Lwinzi Kidiga Musoma, kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono shughuli za Taasisi hiyo, ikiwemo mapambano dhidi ya RUSHWA.
Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hiyo Septemba 23, 2026 kwa niaba ya TAKUKURU, Mkuu wa Wilaya Mhe. Peter Masindi amempongeza Mhe. Lwinzi kwa kujitolea na kushirikiana na taasisi za Serikali katika shughuli zinazolenga kuimarisha uadilifu na mapambano dhidi ya rushwa.
Aidha, Mhe. Masindi ameipongeza TAKUKURU kwa kuwa na moyo wa kutambua na kuthamini juhudi za wadau wanaoshirikiana na taasisi hiyo, akisema hatua hiyo inawapa moyo wananchi kuendelea kujitolea na kushiriki katika shughuli zinazolenga kuleta manufaa kwa jamii.
Ametoa wito kwa taasisi nyingine za Serikali na binafsi kuwa na utaratibu wa kutambua na kuwapa moyo wananchi wanaojitokeza kuunga mkono juhudi zao, akisema kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo na utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Kwa upande wake, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kishapu, Atuganile Stephen, amesema Taasisi hiyo inathamini ushirikiano wa wadau katika kutekeleza majukumu yake, akieleza kuwa Mhe. Lwinzi alionesha ushirikiano mzuri wakati wa maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 18, 2026.
Amesema miongoni mwa shughuli alizoshiriki ni uzinduzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa ya Maafisa Usafirishaji katika Kijiji cha Utemini, ambapo pia alijitolea vifaa kwa ajili ya ujenzi wa kizimba cha klabu hiyo.
“Mhe. Lwinzi amekuwa mdau muhimu katika shughuli zetu. Alijitolea na kutuunga mkono katika shughuli za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, hivyo tumeona ni muhimu kutambua mchango wake,” amesema Atuganile.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mhe. Lwinzi Kidiga Musoma ameshukuru TAKUKURU kwa kutambua mchango wake, akisema ushirikiano kati ya wananchi na taasisi za Serikali ni muhimu katika kufanikisha shughuli za maendeleo na kujenga jamii inayozingatia uadilifu.
Ushirikiano kati ya taasisi za Serikali na wananchi una umuhimu mkubwa katika kuimarisha uwajibikaji, kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao, pamoja na kusaidia taasisi kupata taarifa na ushirikiano unaohitajika katika kutekeleza majukumu yake. Aidha, ushirikiano huo hujenga imani kati ya wananchi na Serikali na kuchochea ushiriki wa jamii katika kulinda rasilimali na maslahi ya umma.
Mkuu wa Taasisi ya kuzia na kupambana na RUSHWA wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Atuganile Stephen kwenye hafla ya kumkabidhi tuzo aliyekuwa Diwani wa Kata ya Maganzo, Mhe. Lwinzi Kidiga Musoma, kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono shughuli za Taasisi hiyo, ikiwemo mapambano dhidi ya RUSHWA Septemba 23,2026
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed
Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na RUSHWA (TAKUKURU) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Legane Manene
Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na RUSHWA (TAKUKURU) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
Feada Mbilinyi


Social Plugin