Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DIWANI KISHAPU AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Diwani wa Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu kwa kipindi cha Januari-Juni 2026 kilichofanyika Julai 3, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama hicho Wilaya

Diwani wa Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Joel Ndettoson, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2026 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Kishapu.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa leo Julai 3,2026 imeonyesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta za elimu, afya, maji, kilimo, mifugo, mazingira na umeme, huku wajumbe wakipongeza hatua zilizofikiwa na kuishauri Serikali kuendelea kuimarisha huduma za afya, elimu, barabara na kuongeza watumishi wa afya.

Sekta ya Elimu

Kata ya Kishapu ina shule 10, zikiwemo shule za msingi 8 na sekondari 2.

Shule ya Sekondari Isoso ilipokea Sh milioni 342 kwa ujenzi wa shule ya awali na msingi, jengo la utawala pamoja na matundu 20 ya vyoo. Hadi sasa Mradi umekamilika kwa asilimia 100.

Shule ya Msingi Isoso ilipokea Sh milioni 71 kwa ujenzi wa madarasa mawili ya awali na matundu sita ya vyoo, ambayo tayari yanatumika mpaka sasa.

Shule ya Msingi Lubaga ilipokea Sh milioni 7.6 kwa ujenzi wa matundu manne ya vyoo vya wanafunzi wa kiume, na mradi huo tayari umekamilika lakini bado unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi.

Kwa upande wa uandikishaji wa darasa la kwanza, shule nyingi zimefikia asilimia 100 isipokuwa Kishapu (96%), Lubaga (94%) na Mwabusiga (66%).

Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2026 hayakuwa na Daraja Ziro, huku Kidato cha Pili kikirekodi wanafunzi 51 wenye Daraja Ziro katika Shule za Sekondari Kishapu na Isoso.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Paul Shagembe akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu kwa kipindi cha Januari-Juni 2026 kilichofanyika Julai 3, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama hico Wilaya

Sekta ya Afya


Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Kikwete ina jumla ya watumishi 135 hadi sasa lakini bado ina upungufu wa watumishi 177, sawa na asilimia 56, hasa katika vitengo vya mionzi, mochwari na uuguzi.Pia tarifa ya hospitali imeeleza kuwa kupanda kwa gharama za mafuta na vifaa tiba pamoja na ufinyu wa bajeti kunaathiri utekelezaji wa baadhi ya shughuli za huduma za afya.


Zahanati ya Lubaga imeainisha mahitaji ya ujenzi/upanuzi wa jengo la Zahanati, ujenzi wa vyoo vya kisasa vya wagonjwa, Ukamilishaji na ukarabati wa nyumba za watumishi, ukarabati wa tanki kubwa la kuvunia maji na kuhifadia pamoja, huduma ya maji ya uhakika ya Ziwa Viktoria na Ujenzi wa shimo la kuhifadhia kondo la nyuma (Placenta Pit) na uzio wake.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Cornel Zengo akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu kipindi cha Januari- Juni 2026 kilichofanyika Julai 3, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama hicho Wilaya

Sekta ya Kilimo

Taarifa imebainisha kuwa wakazi wengi wa Kata ya Kishapu wanategemea kilimo na mifugo, huku changamoto kubwa ikiwa ni uhifadhi usiozingatia viwango vya zao la pamba baada ya kuvuna, jambo linalopunguza ubora wa zao hilo. Hata hivyo, uzalishaji wa pamba umeendelea kuimarika kutokana na juhudi za maafisa ugani na Bodi ya Pamba.

Ushauri wa Wajumbe

Hata hivyo Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu Regina Ndulu ameseha usomaji taarifa huo ni kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho ili kuona namna serikali inatekeleza ilani yake na yote waliyoahidi kwa wananchi huku akiendelea kuhimiza ushirikiano kati ya viongozi wa Chama, Wataalamu pamoja na wananchi ili kufikia maendeleo endelevu.

Kaimu Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Regina Athmani Ndulu akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu kwa kipindi cha Januari-Juni 2026 kilichofanyika Julai 3, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama hicho Wilaya

Wajumbe wamesisitiza kuendelea kutoa elimu ya kilimo bora cha pamba, kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto shule, pamoja na kushirikisha wananchi katika ujenzi wa madarasa, vyoo na zahanati ili Serikali iweze kukamilisha miradi hiyo kwa manufaa ya jamii.

Ikumbukwe kuwa miradi hiyo yote itawanufaisha wananchi wa Kata ya Kishapu yenye jumla ya wakazi wake 17, 572 huku kati yao Wanaume ni 8426 na Wanawake ni 9146 yenye vitongoji Saba (Isoso, Mhunze, Kishapu, Lubaga, Mwabusiga, Mwasele "B" na Lywandu) na shughuli kuu ikiwa ni kilimo, ufugaji, biashara/ ujasiliamali na wachache kuwa ni wafanyakazi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu kwa kipindi cha Januari- Juni 2o26, kilichofanyika Julai 3, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama hicho Wilaya
Diwani wa Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akifuatilia kikao hicho kwa makini








































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com