
Kamati ya Maandalizi ya Samia Kalamu Awards (SKA) 2026 imetangaza kuongeza muda wa kupokea kazi za kushindanishwa kwa siku 14, ambapo sasa waandishi wa habari na wadau wa sekta ya habari watakuwa na fursa ya kuwasilisha kazi zao kuanzia Julai 1 hadi Julai 14, 2026 saa 5:59 usiku.
Awali, mwisho wa kuwasilisha kazi ulikuwa Juni 30, 2026, lakini Kamati imeamua kuongeza muda huo kufuatia maombi kutoka kwa wadau mbalimbali waliotaka kupewa nafasi zaidi ya kukamilisha na kuwasilisha kazi zao.
Kamati imewahimiza waandishi wa habari, wahariri, wachora katuni, maafisa habari, watengenezaji wa maudhui ya kidijitali na washiriki wengine wenye sifa kutumia kikamilifu muda huo wa nyongeza kushiriki katika tuzo hizo.
Samia Kalamu Awards zilianzishwa mwaka 2024 kwa lengo la kutambua na kuhamasisha ubora, weledi na ubunifu katika uandishi wa habari na makala za maendeleo nchini, zikiwa na kaulimbiu ya "Kalamu kwa Maendeleo."
Social Plugin