Hand in Hand Eastern Africa–Tanzania imekutana na viongozi na wadau wa Wilaya ya Kilolo kwa lengo la kujadili fursa za ushirikiano katika utekelezaji wa Mradi wa INUA II, unaolenga kuwawezesha wanawake, vijana na makundi yaliyo katika mazingira ya uhitaji kujenga uchumi endelevu.Wilaya ya Kilolo ni miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa katika minyororo ya thamani ya kilimo cha bustani (horticulture) na ufugaji wa maziwa. Pamoja na uwepo wa rasilimali na fursa hizo, bado jamii nyingi zinakabiliwa na changamoto za ukosefu wa ujuzi, maarifa na mbinu bora za uzalishaji, uchakataji na kuongeza thamani ya mazao pamoja na bidhaa zinazotokana na shughuli hizo.
Katika kikao hicho, wadau walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, jamii na wadau wa maendeleo ili kujenga uwezo wa wananchi kutumia kikamilifu fursa zilizopo, kuongeza kipato na kuboresha ustawi wa maisha yao.
Kupitia Mradi wa INUA II, Hand in Hand Eastern Africa–Tanzania itaendelea kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa pamoja na wadau mbalimbali katika kutoa maarifa, ujuzi na msaada unaohitajika kwa wananchi, kwa lengo la kukuza shughuli za kiuchumi, kuongeza ajira na kuchochea maendeleo jumuishi na endelevu katika Wilaya ya Kilolo.




Social Plugin