Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATAMBI: SIJAVUNJA KATIBA KWA KUPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA SIASA



Na mwandishi wetu, Shinyanga

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema hajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupiga marufuku mikutano ya siasa nchini, akisisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda amani, usalama na maslahi ya wananchi wengi.

Katambi amesema hayuko tayari kuona taifa linaangamia kwa kuacha kundi dogo la watu wenye maslahi binafsi likiendelea kukiuka haki za wananchi wengi.

Ameyasema hayo leo mkoani Shinyanga alipokuwa akizungumza na mamia ya wazee na wanachama wa Baraza la Ushauri la Wazee la Manispaa ya Shinyanga katika maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wazee Duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com