Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA HAJASAHAU 4R KUWEZESHA MARIDHIANO YA KITAIFA



WATANZANIA wanaitakia mema Tanzania wanapaswa kuendelea kutete amaridhiano na amani na kukumbuka kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alishahakikishia Watanzania kuwa msimamo wake wa kuongoza nchi kupitia falsafa ya 4R ambayo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Kujenga Upya Taifa haujabadilika.

Tukumbuke kwamba akipokea ripoti ya Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kutoka kwa Jaji Othman Chande mnamo Aprili 23, 2026, Rais Samia alieleza kuwa yeye bado ni yuleyule aliyeingia madarakani na nia ya kuleta maridhiano ya kweli.

Alisisitiza kuwa anachoomba kutoka kwa viongozi na wananchi ni ushirikiano wa dhati katika kutekeleza falsafa hiyo, akibainisha kuwa umoja ni nguzo muhimu katika kuvuka changamoto zilizojitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi uliopita.

Ni kweli kua falsafa hiyo ya 4R imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo tangu mwanzo wa utawala wake kupitia hatua mbalimbali za kuimarisha demokrasia na haki za binadamu nchini.

Ikumbukwe kuwa Rais Samia amekuwa kiongozi aliyefungua milango ya mazungumzo na vyama vya upinzani, kuwaruhusu wanasiasa waliokuwa nje ya nchi kurejea, na kutoa uhuru mkubwa kwa vyombo vya habari na mikutano ya kisiasa. Aidha, amefanya mageuzi makubwa ikiwemo kuondoa matumizi ya nguvu katika ukusanyaji wa kodi, kugharamia matibabu ya viongozi wa upinzani kama Tundu Lissu, na kuanzisha Tume ya Hakijinai ili kuboresha mfumo wa haki nchini.

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Rais alionyesha uthabiti wake kwa kufuta utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa na kuondoa wakurugenzi wa halmashauri katika usimamizi wa uchaguzi ili kuongeza uwazi.

Licha ya kuwepo kwa kasoro na vurugu zilizoripotiwa katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, Rais Samia anaamini kuwa suluhu pekee ya kudumu ni kuendelea na njia ya maridhiano badala ya uhasama. Maono yake ni kuona Watanzania wanabaki kuwa wamoja na wenye utulivu ili waweze kuendelea na shughuli zao za maendeleo huku wakijenga taifa lenye misingi imara ya haki na ustahimilivu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com