Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WITO WA DHARURA: FAMILIA YAOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA MGONJWA WA SARATANI YA NEVA



Imeandaliwa na Dotto Kwilasa

Familia ya Saidi Mikidadi Abdallah, anayepambana na ugonjwa hatari wa saratani ya neva inawaomba Watanzania wote wenye moyo wa huruma,  kujitokeza kwa haraka kumuokoa ndugu yeo .

Kwa mujibu wa familia, hali ya mgonjwa imeendelea kuwa mbaya siku hadi siku, hali inayohitaji matibabu ya haraka na ya kitaalamu zaidi.

 Madaktari wamethibitisha kuwa matibabu sahihi kwa sasa yanaweza kupatikana nje ya nchi, hususan nchini India, baada ya juhudi za matibabu hapa nchini kushindikana kuleta nafuu.

Familia imeeleza kuwa tayari imefanikiwa kukamilisha baadhi ya taratibu muhimu za safari, ikiwemo kupata visa, lakini bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kifedha kugharamia nauli na matibabu. 

Jumla ya fedha zinazohitajika kwa ajili ya matibabu pekee ni takribani shilingi milioni 40 za Kitanzania, bila kujumuisha gharama za usafiri na malazi.

Kutokana na hali hiyo, familia imeamua kuomba msaada kwa umma ili kuokoa maisha ya mpendwa wao. Wamesisitiza kuwa mchango wowote, mkubwa au mdogo, unaweza kuwa chanzo cha tumaini na uhai kwa mgonjwa.

“Mchango wako unaweza kuleta tofauti kubwa. Tunaomba sana msaada wenu katika kipindi hiki kigumu,” imeeleza familia kwa masikitiko makubwa.

Wanaotaka kuchangia wanaweza kutuma fedha kupitia:

Namba: 0757551443 (Vodacom)

Jina: Radhia Rajabu

Jamii inaombwa kuungana kwa pamoja katika jitihada hizi za kibinadamu, huku dua na michango ikihitajika kwa haraka ili kumpatia Saidi nafasi ya kupata matibabu na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Mungu awabariki wote watakaoguswa na kusaidia katika jitihada hizi za kuokoa maisha ya ndugu yetu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com