Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WACHIMBAJI WADOGO WALIA NA TOZO, DC AAGIZA SULUHISHO NDANI YA SIKU NNE

Na Stella Herman,Shinyanga

Wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa Mwakitolyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga  wamesema  kutozwa tozo mpya ya Sh200,000 kwa kila gari linalobeba mawe kutoka mgodini ni kuwaumiza kutokana na kulipa tozo zingine ambazo ziko kwa mujibu wa sheria.

Hatua hiyo imekuja kufuatia  malalamiko kutoka kwa wachimbaji wadogo mgodi wa Mwakitolyo, waliodai kutozwa Sh 200,00 kwa kila gari linalotoka mgodini likiwa na mawe kwani  hatua hiyo imekuwa mzigo mkubwa unaowaathiri kiuchumi na kudhoofisha shughuli zao za kila siku.

Wakitoa malalamiko yao kwenye kikao cha Mkuu wa Wilaya , wachimbaji wameeleza kuwa pamoja na tozo hiyo mpya, tayari wanakabiliwa na gharama nyingi za uendeshaji ikiwemo mrabaha, huduma mbalimbali, michango ya kijamii pamoja na ada za ukaguzi.

Mchimbaji mdogo Alphonce Magesa, amesema hali ya uzalishaji imekuwa ngumu zaidi kutokana na gharama hizo, akibainisha kuwa mazingira ya mgodi huo yanahitaji uwekezaji mkubwa wa uendeshaji kila siku.

Alieleza kuwa matumizi ya mashine kama greda pamoja na mafuta kwa kiwango kikubwa vinaongeza mzigo, hali inayowafanya wachimbaji kushindwa kupata faida inayotarajiwa .

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akiwa ameshika nyaraka ya halmashauri ya Shinyanga ambayo ilipitishwa na baraza la madiwani kuidhinisha tozo ya Sh 200,000 kwa kila gari lililobeba mawe linalotoka mgodi wa Mwakitolyo.
Alice Kianila akiwasilisha madai ya wachimbaji wadogo wanawake juu ya tozo mpya ya Sh 200,000 kwa kila gari

Mwanasheria wa halmashauri ya Shinyanga akitoa ufafanuzi

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wilayani humo, Elias Amos, amesema suala la tozo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu, hivyo kuhitaji uamuzi wa haraka wa mamlaka husika.

Akifafanua zaidi, Mtatiro amesema tozo hiyo ilipitishwa na Kamati ya Fedha na Mipango mwaka 2022 na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani kabla ya kuanza kutekelezwa mwaka huu,ambapo ametoa maagizo ipitiwe upya ili kuondoa malalamiko.

Amesema  lengo la Serikali si kuwaumiza wananchi bali kuhakikisha kunakuwa na uwiano kati ya ukusanyaji wa mapato na ustawi wa wadau wa sekta ya madini.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com