Hatua ya Tundu Lissu kuonesha utayari wa kushiriki mazungumzo ya kitaifa imeendelea kuibua matumaini ya maridhiano, huku ikitafsiriwa kama fursa muhimu ya kuimarisha mshikamano wa Taifa na misingi ya demokrasia nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mwanachama na aliyekuwa mgombea wa Uenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa 2015, Odero Charles Odero, ametoa wito kwa wanasiasa na wanaharakati kuunga mkono mchakato huo kwa njia chanya, akisisitiza umuhimu wa kuepuka kauli au vitendo vinavyoweza kuchochea migawanyiko, chuki na uhasama.
Odero amesema wanaharakati wanapaswa kutumia nafasi na ushawishi wao kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mazungumzo ya maridhiano, badala ya kuingilia au kupotosha mwelekeo wa juhudi hizo, akibainisha kuwa umoja wa kitaifa unapaswa kupewa kipaumbele kuliko misimamo mikali ya kisiasa.

Social Plugin