Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUTOKA MAKTABA: KAULI HIZI ZA KICHOCHEZI TUZIKATAE



Na mwandishi wetu

Wanazuoni na wachambuzi wa siasa wanaonya na kusisitiza kuwa ni muhimu wananchi kuwa waangalifu na kuwakataa wanasiasa wanaotumia majukwaa mbalimbali ya kisiasa kueneza chuki na uchochezi kwenye jamii kwani kauli hizo ni hatari na zinaweza kukuza uhasama kwenye jamii na kuvuruga utulivu na amani iliyopo nchini Tanzania.

Kauli hizo kulingana na wanazuoni na wachambuzi hao, zinachochea uasi na kupunguza matumaini ya wananchi katika utawala wa kidemokrasia, zikienda pia kinyume na maslahi ya Taifa, wajibu wa kila Mtanzania ukielezwa kuwa ni kupinga kauli za aina hiyo, wito ukitolewa wa kutafuta njia mbadala na mabadiliko ya kisiasa kupitia mifumo rasmi ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa kidemokrasia.

"Huu ni wakati wa kuwakataa wanasiasa hawa ambao hawana cha kupoteza, kushikamana na kupinga kauli na vitendo vyote vitakavyohatarisha amani, utulivu na maendeleo yetu. Wanasiasa wanapaswa kuelewa kuwa majukumu yao ni kutafuta njia bora za kutatua changamoto za kisiasa kwa kutumia mifumo rasmi na ya kisheria na si kwa kuchochea hasira, vurugu na uasi kama ilivyokuwa wakati wa kampeni ya Chama kimoja ya No Reforms, No election ambapo walisikika kabisa wakitaka kufanya uasi." Amesema Bw. Erasto Katunzi, Mchambuzi wa masuala ya siasa.

Ingawa ni haki ya Kidemokrasia kudai mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, njia iliyohubiriwa ya kutumia uasi imetajwa kuwa hatari zaidi kwa usalama wa raia na mali zao, ikielezwa kuwa kauli hizo zinazochochea wananchi kuasi mamlaka au kuzuia michakato ya kisheria na kidemokrasia zinaweza kulipeleka Taifa katika machafuko ambayo yakianza hayachagui ni nani wa kumuathiri.

Mchambuzi Allen Mwambene anasema madhara ya kauli kama zilizowahi kusemwa na Viongozi wakuu wa Chadema zinatishia kuvunjika kwa umoja wa Kitaifa na kusambaratika kwa amani ya Nchi, akisisitiza umuhimu wa wamanchi kutokubali kutumika kama daraja la wanasiasa kufikia malengo yao kwa gharama za kumwaga damu, akisema mageuzi ya kweli yanapatikana kwa mazungumzo ya Kitaifa na ushiriki wa kidemokrasia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com