Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HATUA YA TUNDU LISSU YAIBUA MATUMAINI YA MAZUNGUMZO YA KITAIFA



Hatua ya Tundu Lissu kuonesha utayari wa kushiriki mazungumzo ya kitaifa imeibua matumaini mapya ya maridhiano, ikitazamwa kama fursa ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa na misingi ya demokrasia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 20, 2026 mwanachama na aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Odero Charles Odero ametoa wito maalum kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukubali ombi la Lissu, akisisitiza kuwa hatua hiyo itafungua ukurasa mpya wa mazungumzo na kurejesha imani ya kisiasa miongoni mwa wadau.

Ameeleza kuwa kukubaliwa kwa ombi hilo, ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto za kisheria zinazomkabili Lissu, kutasaidia kuweka mazingira bora ya mazungumzo yenye tija yatakayolenga kumaliza tofauti za kisiasa kwa njia ya amani na ustaarabu.

Hata hivyo, Odero amesisitiza kuwa mafanikio ya mchakato huo yanategemea dhamira ya kweli ya pande zote, akiwataka viongozi na wadau wa kisiasa kuacha misimamo mikali na badala yake kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com