Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FAMILIA ZAHIMIZWA KUWAJIBIKA KULEA VIJANA KATIKA MAADILI NA KUMJUA MUNGU



Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam leo Jumamosi Aprili 04, 2026 wameendelea kusisitiza umuhimu wa familia kuelimisha watoto na Vijana wao kuhusu umuhimu wa amani, wakisisitiza pia wajibu wa wazazi kulea watoto katika maadili mema na maisha yenye hofu ya Mungu na yaliyojaa uelewa kuhusu masuala ya dini.

Wananchi hao akiwemo Bi. Cecilia Maganga, Mkazi wa Kigogo Fresh na Bw. Ibrahim Seif Wambura wamesisitiza pia umuhimu wa amani nchini, wakibainisha kuwa amani ndiyo imekuwa msingi wa maendeleo na ustawi wa Jamii na mwananchi mmoja mmoja kwani amani ndio inayoruhusu wananchi kufanya shughuli zao bila wasiwasi.

"Sisi kama familia tunatakiwa kukaa na watoto na Vijana wetu majumbani, tuwaelimishe kuhusu amani na umuhimu wa kuilinda amani ya nchi na ilivyo gharama kubwa zaidi kuirejesha ikiwa itapotea. Sisi katika dini tunaamini Imani hii ni Mungu ametupa kwahiyo tuwaelimishe pia watoto wetu kuhusu dini. Amani ni kila kitu na ndio inatupa uhuru wa kufanya shughuli zetu bila ya hofu." Amesema Bi. Cecilia Maganga.

Kwa upande wake Bw. Wambura ameonya kuhusu Vijana kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani nchini pamoja na kushiriki katika kupanga na kuratibu maandamano yasiokuwa rasmi na kutokushawishiwa kufanya vurugu nchini, akiwataka Vijana kutumia vyema amani, usalama na utulivu uliopo nchini katika kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya shughuli zilizo halali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com