Na Barnabas Kisengi Dodoma
Wananchi wa Mtaa wa image kata ya kilimani Jijini Dodoma wamelalamikia mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira (Duwasa) pamoja na kampuni inayokusanya takataka katika mtaa wa Image pamoja na wakala wa barabara za Mjini na vijijini (Tarura) kwa ubovu wa miundombinu ya barabara za Mtaa wa Image.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mhe Diwani wa kata ya kilimani Jijini Dodoma wamesema kuwa wamekuwa na kero kubwa ya kupasuka kwa Bomba kubwa ambalo limekuwa likivujisha maji ambayo yamekuwa yakimwagika na kuleta hasara katika makazi yao licha ya pia kuwa ni upotevu wa maji katika eneo hilo ambayo ni hasara kwa mamlaka hiyo pia wamezungumzia changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu ya barabara za mitaa huo pamoja na kuwekewa Taa za barabarani katika Mtaa huku wakilalamikia miundombinu ya barabara za mtaa huo kuwa ni mbovu jambo linalowapelekea wakishindwa kupita na vyombo vya usafiri kama magari na bajaji mtaani hapo.
"Hili swala la bomba kupasuka limekuwa kero kubwa kwetu licha ya kutoa taarifa kwenye mamlaka husika pamoja na wataalamu wa Duwasa kufika lakini hatujaona hatua zozote zilizo chukuliwa hadi Sasa jambo ambalo tunalihofia kuwa bomba hili likizudi kupasuka litaleta athari kubwa katika makazi pamoja na hizo changamoto bado tunachangamoto nyingine ya miundombinu ya barabara za mtaa wetu sio rafiki jambo ambalo wakazi wenye vyombo vya usafiri kama magari na bajaji kushindwa kuingia katika baadhi ya maeneo yetu kwenye mtaa hata tunapo kuwa na mgonjwa huwa ni shida kuingia katika maeneo yetu ya mtaa wetu amesema moja wa wananchi akiwawakikisha Wananchi wenzake katika mkutano wa hadhara wa Mhe Diwani wa kata hiyo hivyo tunaomba sana Mhe Diwani na wataalamu wako tena tumeona viongozi wa chama hapo mtusaidie kutatua changamoto hizi kwetu imekuwa kero ya muda mrefu licha ya kuripoti kwa viongozi wetu wa mtaa sasa tunaamini kuwa viongozi wa CCM kata na wataalamu kutoka kata sasa tunaamini kuwa tutapata ufumbuzi wa changamoto zetu za Mtaa kushulikiwa Ipasavyo.amesema moja wa wananchi akiwawakikisha Wananchi wengine Mzee Sebastian Chambasi
Aidha wananchi hao wakatoa changamoto nyingine za uwepo wa takataka kwa muda mrefu ambazo hazijachukuliwa kwa muda mrefu licha ya wao kuchangia pesa jambo ambalo ni hatari linaloweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kulalamikia kuwepo kwa mtaro ambao umekuwa na Mamba ambao wamekuwa wakionekana mara kwa mara huku watoto wakiwa wanapita kwenye mtaro huo ambao ni hatari kwa maisha ya watu wanao pita kwenye mtaro huo hivyo wameomba wahusika wafuatilie swala hilo kwa uharaka.
Akijibu changamoto hizo Diwani wa kata ya kilimani Jijini Dodoma Mhe Mussa Mkunda amesema kuwa changamoto zote hizo amezichukuwa na wanakwenda kuzifanyia kazi kwa haraka ili kuleta tija kwa wananchi wa Mtaa wa image huku akimwelekeza afisa mifugo wa kata Bi Tabia Shani kuwasiliana haraka na watu wa maliasi ili kuweza kutatua changamoto hiyo kwa haraka ili isije ikasababisha maafa katika mtaa huo kutokana na wananchi wanao vuka katika korongo hilo.
"Ndugu zangu wananchi wa mtaa wa image niwapongeze sana kwa kuweza kuelezea changamoto za mtaa wenu niwahakikishie Mimi kama Diwani wenu hapa zimefika na tunakwenda kuzifanyia kazi kwa haraka nitahakikisha Mimi na wataalamu wangu tulio ongozana nao na viongozi wa Chama cha mapinduzi ambao ndio tunatekeleza ilani tunazifanyia kazi ikiwemo kuwafukia wahuusika wote kwa haraka ili kuhakikisha changamoto zote mlizo sema zinafanyiwa kazi kwa haraka na kuleta tija kwenye Mtaa huu niwaahidi kwakuwa nimeongozana na wataalamu na viongozi wa chama tutahakikisha tumemaliza hizi changamoto zote za Mtaa naomba muendelee kuniamini Mimi ni Diwani niliyotokana na chama cha mapinduzi hivyo kwenu lazima niwe msikivu na kwakuwa tunatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ndio maana nimeongoza na viongozi wa CCM hapa pamoja na wataalamu"amesema Diwani wa kata ya kilimani Mhe Mussa Mkunda
Kwa upande Wake katibu wa chama cha mapinduzi CCM kata kilimani Ramadhani Ramadhani amesema kuwa kama chama ndicho chenye ilani inayotekelezwa kwa kipindi Cha 2025/2030 wao kwa kushirikiana na serikali watahakikisha changamoto zote zilizojitokeza kwenye mkutano huo zinafanyiwa kazi kwa haraka ili kuweza kuhakikisha wananchi wanakuwa katika mazingira mazuri na salama kwenye Mtaa huo.
Ziara hiyo ya Mhe Diwani wa kata ya kilimani ya Mtaa kwa mtaa imeanza katika mtaa wa Image na itaendele katika Mtaa wa kilimani, Nyerere na itamalizika katika Mtaa wa Chinyoyo ikiwa na lengo kuu la kuongea na Wananchi wa Mtaa husika kusikiliza changamoto mbalimbali zilizop kwenye mitaa minne ya kata ya kilimani Jijini Dodoma.
Ziara hiyo ya Mhe Diwani imewashirikisha viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kata ya kilimani wakimbatana na wataalamu kutoka ofisi ya Mtendaji wa kata ya kilimani ikiongozwa na Mtendaji wa kata ya kilimani akiongozana na wataalamu wake afisa afya ,afisa maendeleo ya jamii,afisa mifugo,Police kata na watendaji wa mitaa yote minne ya kata ya kilimani pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya kilimani Jijini Dodoma.



Social Plugin