
Mganga Mkuu wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,Dk. Yudas Ndungile,akizungumzia kampeni ya polio mkoa wa Shinyanga.

Mwakilishi Wizara ya afya ,idara kinga na elimu ya afya kwa umma,Anne Shuma akizungumza na vyombo vya habari.

Mganga Mkuu wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,Dk. Yudas Ndungile,akizungumzia kampeni ya polio mkoa wa Shinyanga.

Mratibu Elimu ya afya kwa umma Mkoa wa Shinyanga, Moses Mwita, akiongea na vyombo vya habari.
Na Mwandishi wetu
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuelimisha umma kuhusu kampeni ya chanjo ya polio inayotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 24 hadi 27 mwaka huu.kampeni hiyo itahusisha utoaji wa chanjo kwa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 10, ambapo chanjo itatolewa bure kwa njia ya matone mawili ya mdomoni.
Akizungumza katika mafunzo hayo leo machi 17,2026, Dk. Yudas Ndungile, amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha watoto wote wanapatiwa chanjo ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa wa polio, huku akisisitiza ushiriki wa jamii nzima ni muhimu kufanikisha zoezi hilo.
"Tunaamini nguvu ya vyombo vya habari katika kuwafikia wananchi kwa haraka na wigo mkubwa na kwa utoaji wa taarifa zenye usahihi wa kutosha kupitia mafunzo haya leo kwa ajili ya kampeni hii ya chanjo ndani ya mkoa wetu ,vyombo vya habari ni daraja muhimu kwa upelekaji wa taarifa za serikali zilizo sahihi"amesema Ndungile.
Kwa upande wake,Mratibu Elimu ya afya kwa umma Mkoa wa Shinyanga, Moses Mwita, ameeleza kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kufikisha ujumbe sahihi kwa wananchi, hivyo ni muhimu kutumia taaluma yao kuhamasisha wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo.
"Nyie ni kundi muhimu la kuwafika wanachi kwa haraka zaidi kwa kuwa na ujumbe sahihi kupitia kalamu zenu"amesema Mwita.
Naye ,Mwakilishi Wizara ya afya ,idara kinga na elimu afya kwa umma,Anne Shuma amefafanua kuwa chanjo ya polio ni salama na imeidhinishwa kitaalamu, akibainisha kuwa hakuna madhara kwa watoto, hivyo jamii inapaswa kuondoa hofu na kujitokeza kikamilifu.
Pia, Shuma alieleza kuwa kampeni hiyo inalenga kuwafikia zaidi ya watoto milioni 6 kitaifa, huku Mkoa wa Shinyanga ukitarajiwa kuwafikia watoto zaidi ya laki 7. Mikoa mingine itakayohusika ni pamoja na Geita, Mwanza, Simiyu, Mara, Tabora na Singida.
"Serikali imechukua hatua madhubuti ya kukinga wananchi wake dhidi ya maambuki ya polio na kila mwananchi atapata huduma bure ndani kaya yake na kila mtoto atawekewa alama kwa kidole baada ya kupata chanjo"amesema Shuma
Mafunzo hayo yamelenga pia kuwapa waandishi uelewa sahihi kuhusu masuala ya chanjo ili waweze kuandika habari zenye usahihi na ushawishi kwa jamii, hususani katika kipindi hiki cha kampeni.
Waziri wa Afya atazindua wa kampeni hiyo kitaifa katika Mkoa wa Mwanza ambapo huku Mkoa wa Shinyanga ukitarajiwa kuwa miongoni mwa mikoa itakayofanya vizuri katika utekelezaji wake.


Waandishi wa habari wakifatilia mafunzo ya chanjo ya polio.
Mwakilishi wa Wizara ya afya idara ya kinga na elimu kwa umma akitoa maelezo.
Mwakilishi wa shirika la Red cross mkoa wa Shinyanga.


Social Plugin